30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

NFRA kuyafikia maeneo yenye uhitaji wa chakula nchini

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula(NFRA) umejipanga kuhudumia maeneo  yatakayothibitika kuwa na mahitaji ya dharula au upungufu wa chakula.

Hayo yameelezwa Oktoba 22, 2022 Jijini hapa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala huo , CPA. Milton Lupa wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu shughuli za zinazofanywa na wakala huo pamoja na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa Fedha 2022/23.

Afisa huyo amesema Ili kuongeza uwezo wa kuhifadhi chakula nchini,wakala  unatekeleza mradi wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka,ambapo ukikamilika utaongeza uwezo wa kuhifadhi kutoka tani 251,000 hadi tani 501,000.

“Tumemejipanga kuhudumia maeneo  yatakayothibitika kuwa na mahitaji ya dharura au upungufu wa chakula kwani hiyo ni moja ya kazi zetu,”alisema Afisa Mtendaji huyo.

Hata hivyo, ametoa wito kwa wananchi kujihakikishia usalama wa chakula kuanzia ngazi ya Kaya,wahifadhi akiba ya kutosha ya chakula kipindi cha mavuno na kuuza chakula pale wanapokuwa na ziada katika uzalishaji.

Lupa amesema kuwa NFRA imefanikiwa kukamilisha sehemu ya mradi na kuongeza uwezo wa kuhifadhi kwa tani 90,000 katika kanda za Arusha (Halmashauri ya Babati) na Sumbawanga na Mpanda.

Amesema kukamilika kwa mradi huo kumeongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka kutoka tani 251,000 hadi tani 341,000 na utekelezaji wa Mradi katika maeneo mengine Dodoma, Songea,Shinyanga,Songwe na Makambako umefika asilimia 85,”amesema Lupa.

Amesema NFRA imefanikiwa kutoa ajira za muda mfupi kwa wananchi zaidi ya 3,000 zinazochangia kipato kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Lupa amesema Ajira hizo zinatokana na kazi mbalimbali zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa zoezi la ununuzi wa nafaka, uhifadhi na kipindi cha uzungushaji wa nafaka na utekelezaji wa Mradi wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka.

Amesema ili kukabiliana na makali ya mfumuko wa bei za nafaka Wakala kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo imeongeza upatikanaji wa nafaka katika masoko ili kuleta unafuu wa maisha kwa wananchi.

“Wakala unahudumia Halmashauri za Bunda,Sengerema, Geita, Nzega,Liwale, Nachingwea, Longido, Loliondo na Monduli ambapo takriban tani 3,000 zimepelekwa katika maeneo hayo,” amesema Lupa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles