24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

TEVEZ AMALIZANA NA SHANGHAI SHENHUA

SHANGHAI, CHINA


tevezz

MATAJIRI wa klabu ya Shanghai Shenhua ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini China, tayari wamemalizana na nyota wa zamani wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Argentina, Carlos Tevez, kwa kumsajili kwa kitita cha pauni 615,000 sawa na zaidi ya bilioni 1 kwa wiki.

Nyota huyo kwa sasa ameweka historia ya mchezaji ambaye analipwa fedha nyingi duniani kutokana na kukamilika kwa uhamisho huo baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Boca Juniors ya nchini Argentina.

Tevez mwenye umri wa miaka 32, atakuwa anachukua kitita cha 1,604,730,00 kwa wiki, huku akiwafunika nyota wa soka duniani, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Lionel Messi wa Barcelona, ambao wanachukua kitita cha pauni 365,000 kwa wiki sawa na Sh 952,403,000.

Tevez ambaye amewahi kukipiga katika klabu ya West Ham, Manchester United na Manchester City, tayari amekamilisha hatua za awali na anatarajia kujiunga na wachezaji wenzake wa klabu hiyo kwa ajili ya mazoezi.

Baada ya kukamilisha dili hilo, Tevez anatarajia kukutana na kocha wa timu hiyo, Gustavo Poyet, ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea na Tottenham huku akicheza nafasi ya kiungo enzi hizo.

Klabu ya Boca Juniors ambayo ametoka Tevez, imetumia mtandao wao wa kijamii kumtakia kila la heri mchezaji huyo katika maisha yake mapya ya soka nchini China.

“Tunakutakia kila la heri Carlitos, siku zote utaendelea kuwa katika mioyo yetu, tunathamini mchango wako kwetu na tunajua utaendelea kufanya yale ambayo ulikuwa unayafanya hapa,” waliandika.

Mchezaji huyo baada ya kujiunga na Boca Junior wakati wa majira ya joto msimu uliopita, hadi leo hii anaondoka amefanikiwa kufunga mabao 25 katika michezo 56 aliyocheza, huku akiisaidia klabu hiyo kutwaa taji la Argentina Primera Division na Copa Argentina.

Kwa upande wa klabu ya Shanghai Shenhua, imepambana na kumaliza nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi nchini China ambapo ilikuwa na wachezaji ambao waliwahi kuwika katika soka duniani kama vile nyota wa zamani wa Chelsea, Demba Ba, mchezaji wa zamani wa Newcastle United, Obafemi Martins na nyota wa zamani wa Inter Milan, Fredy Guarin.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles