30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Tenki la majitaka feri lapasuka

znz-17

Na FERDNANDA MBAMILA-DAR ES SALAAM

Tenki la kuhifadhia majitaka katika Soko la Kimataifa la Samaki (Feri),  limepasuka na hivyo kukabiliwa na changamoto za kulipuka kwa magonjwa ya mlipuko.

Akizungimza na MTANZANIA, Mwenyekiti  wa Soko hilo , Omary Mtolea, alisema tatizo la miundombinu ni changamoto inayolikabili soko hilo kwa muda mrefu.

Mtolea alisema jambo hilo limesababisha chemba moja kupasuka na kumwaga maji hayo machafu nje ya utaratibu.

Alisema baada ya kuona tatizo linazidi kuwa kubwa waliamua kupeleka malalamiko yao Halmashauri ya Ilala ambao waliahidi kulitengeneza, lakini hadi sasa hawajaona jitihada zozote kunusuru afya za wadau wa soko hilo.

“Mkandarasi anayesimamia usafi na ushuru katika soko hilo, anatarajia kumaliza mkataba wake ifikapo Desemba mwaka huu.

“Hivyo tutajipanga upya jinsi tutakavyoona inafaa ikiwa ni pamoja na kufanya tathimini kuweza kujiridhisha kama anaweza kuendelea au kuachia ngazi,”alisema Mtolea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles