23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Homa ya ini tishio kuliko Ukimwi

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ini na Matumbo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), John Rwegasha
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ini na Matumbo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), John Rwegasha (Kulia)

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

KASI ya maambukizi ya virusi vya homa ya ini (Hepatitis B) nchini ni kubwa ikilinganishwa na ile ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi, imeelezwa.

Inakadiriwa kuwa watu wanane kati ya 100 hukutwa na maambukizi hayo, kiwango ambacho ni kikubwa zaidi ya kile kinachokadiriwa kwenye VVU ambacho ni asilimia pungufu ya sita.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ini na Matumbo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), John Rwegasha, alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma ya uchunguzi na tiba dhidi ya ugonjwa huo inayotarajiwa kuanza kutolewa hospitalini hapo.

Dk. Rwegasha alisema licha ya hatari kubwa na kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo, bado kuna changamoto kubwa ya uelewa kwa jamii ikilinganishwa na ugonjwa Ukimwi, kifua kikuu na magonjwa mengineyo yanayoambukiza.

“Ugonjwa wa homa ya ini husababishwa na kirusi kiitwacho Hepatitis B.

“Njia za maambukizi zinashabihiana na zile za Ukimwi ikiwamo kufanya ngono zembe, kuchangia vitu vyenye ncha kali, kupewa damu isiyopimwa na kupitia uzazi wa mama na mtoto hasa wakati wa kujifungua,” alisema.

Daktari huyo alisema kama ilivyo kwa   Ukimwi, ugonjwa sugu wa homa ya ini hauna tiba ya kuuponya isipokuwa dawa zilizopopatikana hadi sasa zinaweza kupunguza kasi ya maambukizi mwilini na kuzuia madhara zaidi kwenye ini.

“Ugonjwa wa homa ya ini usipotibiwa matokeo yake husababisha saratani ya ini.

“Hapa Muhimbili asilimia 60 ya wagonjwa wanaokutwa na saratani ya ini mara nyingi imetokana na maambukizi ya virusi hivi,” alisema.

Dk. Rwegasha alisema ndiyo maana hushauriwa mtu yeyote aliyepatwa na ugonjwa huo kutumia dawa muda usiopungua miaka mitano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles