27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

Kijana mrefu sasa kupata matibabu Tanzania

Baraka Elias
Baraka Elias

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

BARAKA Elias (35), kijana mwenye urefu wa futi 7.4 anayesubiri kufanyiwa matibabu ya kubadilisha nyonga yake ambayo imevunjika, hatapewa tena rufaa ya kwenda nje ya nchi kufuata matibabu hayo.

Badala yake atafanyiwa upasuaji katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) ambako anapatiwa matibabu ya kutuliza maumivu yanayomkabili hivi sasa.

Mkurugenzi wa MOI, Dk. Othuman Kiloloma alisema hayo jana alipozungumza na MTANZANIA.

Gazeti hili  lilitaka kujua hatma ya matibabu ya kijana huyo ikizingatiwa awali MOI ilishindwa kumfanyia upasuaji huo kutokana na umbile lake.

Ilielezwa kwamba madaktari walishindwa kumtibu kwa sababu mashine za MOI hazikuwa zinalingana na urefu wake.

Mkurugenzi huyo alisema baada ya changamoto hiyo kujitokeza, walilazimika kuunda jopo la madaktari ambalo lilifanya tathmini ya matibabu ya kijana huyo.

“Kwa kuwa umbo lake ni kubwa ikilinganishwa na watu wengine, tulipokwama awali ilitulazimu kuunda jopo la madaktari kufanya tathmini na uamuzi wa hatma ya matibabu ya Elias.

“Jopo hilo lililokuwa likiongozwa na Daktari wetu, Lupondo, tayari limefanya tathmini na imeonekana kwamba kifaa anachohitaji kinaweza kupatikana, hivyo badala ya kumpa rufaa kwenda nje tumewasiliana na nchi tatu  tupate kifaa hicho,” alisema.

Dk. Kiloloma alitaja nchi ambazo wamewasiliana nazo  kupata kifaa kinachohitajika kufanikisha upasuaji huo kuwa ni Ujerumani, Marekani na India.

“Hawa wana viwanda vinavyotengeneza kifaa hicho kwa ubora, hatujajua hadi kitakapofikishwa hapa kitagharimu kiasi gani itategemeana na bei ya ununuzi.

“Na kwa sababu ya umbile lake watalazimika pia kubadilisha kidogo mfumo wa mashine zao  kupata kile kitakachomtosheleza mgonjwa wetu… kwa hiyo bado hatujajua pia kitawasili lini nchini,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles