23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mauzo ya hisa yazidi kushuka

 Ofisa Mwandamizi wa Masoko wa DSE, Mary Kinabo
Ofisa Mwandamizi wa Masoko wa DSE, Mary Kinabo

Na JOHANES RESPICHIUS -DAR ES SALAAM

MAUZO katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) yameshuka kwa asilimia 87 kufikia Sh milioni 500 kutoka Sh bilioni 4 wiki iliyopita. Wiki iliyopita yalishuka kwa asilimia 37.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana, Ofisa Mwandamizi wa Masoko wa DSE, Mary Kinabo, alisema idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imepungua kwa asilimia  85 hadi kufikia 1.02 kutoka 6.72 wiki iliyopita.

Mary alisema kushuka huko kunaweza kuhusishwa na ongezeko la mauzo ya hati fungani ambazo wiki hii zimeuzwa nne na kununuliwa kwenye soko kwa thamani ya Sh bilioni 22.1 sawa na asilimia 33.

“Wiki iliyopita ziliuzwa na kununuliwa hati fungani sita kwa thamani ya Sh bilioni 16.6, hivyo inawezekana wawekezaji wamehamia katika kuwekeza katika upande huo na kuacha kuwekeza katika hisa.

“DSE imeongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa kwa asilimia 37.74 kutoka asilimia 6.44 wiki iliyopita, ikifuatiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa asilimia 21.39 kutoka asilimia 2.18 na CRDB kwa asilimia 13.33 kutoka 41.40 wiki iliyopita.

“Ukubwa wa mtaji wa soko nao umeendelea kushuka. Wiki hii umeshuka kwa asilimia 2.5 na kufika Sh trilioni 20.4 kutoka Sh trilioni 20.9 wiki iliyopita baada ya wiki hiyo kushuka kwa asilimia 2.4.

“Ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani umeendelea kubaki kwenye kuwango kile kile cha Sh trilioni 8.14,” alisema Mary.

Kwa upande wa viashiria vya soko, Mary alisema sekta ya viwanda imeendelea kubaki kwenye wastani ule ule wa Sh 5.031 huku sekta ya huduma za benki na fedha ikishuka kwa pointi 0.52 baada ya bei za hisa za DSE kushuka kwa asilimia 1.59 na sekta ya huduma za biashara ikibaki kwenye wastani wa Sh 3,157.95.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles