27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Teknolojia mpya kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa utumbo nje

AVELINE KITOMARY, DAR ES SALAAM

Madaktari bingwa wa upasuaji wa watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), kwa mara ya kwanza wamefanikiwa kuokoa maisha ya watoto wawili waliozaliwa wakiwa na tatizo tumbo kuwa wazi na utumbo kuwa nje kwa kitaalamu Gastroschisis.

Hatua hiyo imetokana na utaratibu wa kuwavalisha mifuko maalumu ambayo haihusishi mtoto kufanyiwa upasuaji wala kupewa dawa za usingizi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Aprili 16, daktari bingwa wa upasuaji wa watoto, Zaituni Bokhary amesema awali kabla ya teknolojia hiyo kuwepo uwezekano wa watoto wanaozaliwa tumbo wazi na utumbo nje kufariki ulikuwa ni asilimia 100 lakini hivi sasa uwezekano wa kupona ni asilimia 100.

“Kabla ya teknolojia hii watoto wenye tatizo hili ilibidi wafanyiwe upasuaji na kuvalishwa mifuko ya kawaida ambayo ufanisi wake ulikuwa mdogo na ulihusisha kupitia taratibu mbalimbali za upasuaji ikiwamo kupewa dawa za usingizi ambapo kutokana na uchanga wa watoto na muda ulikuwa unatumika kurejesha matumbo watoto walipata madhara mbalimbali ikiwamo vifo.

“Kuanzia sasa mtoto akizaliwa na tatizo hili atavalishwa mfuko maalumu unaotunza majimaji akiwa wodini ambapo kila siku watoa huduma watakua wanausukuma utumbo kurudi tumboni kwa vipimo maalumu na katika kipindi cha siku tatu hadi tano utumbo huo utakuwa umerudi ndani kwenye hali ya kawaida.

“Baada ya hapo mtoto atafungwa tumbo kwa njia maalumu ambayo haiusishi kushonwa na nyuzi,” amesema Dk. Bokhary.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles