26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Watatu mbaroni Dar kwa kukutwa na heroin kilo 270

 CHRISTINA GAULUHANGA – DAR ES SALAAM 

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, inawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kukutwa na kilo 270 za dawa za kulevya aina ya heroin. 

Waliokamatwa ni raia wa Nigeria, David Chukwu (39), raia wawili waTanzania akiwamo Mkutubi wa Chuo Cha Aga Khan jijini Dar es Salaam, Alistair Mbele (38) ambaye ni mkazi wa Mbezi Kibanda Cha Mkaa na Isso Lupembe (49) mkazi wa Changangikeni. 

Katika taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari, Kaimu Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo, James Kaji, alisema watuhumiwa hao walikamatwa juzi baada ya kuwekewa mtego ulioshirikisha vikos vya usalama vya ndani na nje. 

Alisema watuhumiwa hao kabla ya kusafisha mzigo huo kutoka nje, walianza kujenga chemba ya choo ‘karo’ ili wahifadhie dawa hizo zitakapofika. 

Kaji alisema kabla ujenzi wa karo hilo kwisha, dawa hizo zilifika nchini wakakosa sehemu ya kuzihifadhi na hivyo kuamua kuziweka ndani ya nyumba. 

“Tunashukuru tulikuwa tunashirikiana na vikosi mbalimbali vya nje ya nchi ambavyo vinapinga matumizi ya dawa hizi na vya hapa nchini na tulifanikiwa kuwanasa wakiwa na mzigo huo huko Mbezi Kibanda cha Mkaa,”alisema Kaji. 

Alisema walikuwa wakiwafuatilia watuhumiwa hao tangu Aprili 8, ambayo walianza kusafisha mzigo huo.

Kaji alisema mamlaka hiyo itaendelea kuwasaka wote wanaojihusisha na biashara hiyo ambayo inaichafua jina la nchi. 

Alitaka jamii kuwafichua watu wanaowashtukiwa kuwa wanaojihusisha na biashara hiyo haramu. 

Upelelezi unaendelea na watuhumiwa watafikishwa Mahakamani wakati wowote. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles