27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

TCRA yatoa mwezi mmoja wamiliki vyombo vya habari mtandaoni kujisajili

Derick Milton – Simiyu

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), Kanda ya ziwa imetoa muda wa mwezi mmoja kwa wamiliki wote wa Blogu, Majukwaa mtandaoni (online forums), Radio na Televisheni za mtandaoni kuhakikisha wanasajili huduma hizo kama sheria inavyotaka.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Injinia Francis Mihayo, wakati akongea na Mtanzania Digital kwenye manesho ya Nanenane Kitaifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Injinia Mihayo amesema kuwa kwa mujibu wa Kanuni ya nne ya maudhui  mtandaoni ya Mwaka 2018 (The Electronic Postal Communications (online content) Regulations, 2018) wamiliki wa forumu hizo wanatakiwa kuzisajili kama inavyotakiwa.

Amewataka wamiliki ambao bado wapo na wanaendelea kutoa huduma, kuhakikisha wanatekeleza sheria hiyo ndani ya mwezi mmoja na endapo watakaidi hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

“Bado wapo wamiliki wa blogu, majukwaa mtandaoni (online forums), radio na televisheni za mtandaoni wanaendelea kutoa huduma bila ya kusajili foramu zao hizo, mamlaka inawataka ndani ya mwezi mmoja kuhakikisha wanasajili kama inavyotakiwa,” amesema.

Akizungumzia zoezi la usajili wa laini kwa alama za vidole, amesema kuwa zeozi hilo linaendelea vizuri huku akiwataka wananchi kuhakikisha wanasajili laini zao kabla ya Desemba 31, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles