Gucci Mane akubali kuhudumia mtoto

0
1571

NEW YORK, MAREKANI

RADRIC DAVIS ‘Gucci Mane’, amefikia makubaliano na mama wa mtoto wake, Sheena Evans, kulipa dola za Marekani 10,000 kila mwezi ambazo ni zaidi ya milioni 22 za Bongo kwa ajili ya huduma za mtoto wao Keitheon.

Wawili hao walifikishana mahakamani mwishoni mwa wiki iliyopita na mahakama ikamtaka rapa huyo kuhakikisha anatoa kiasi hicho cha fedha na atakuwa anarekodiwa pia kumwona mtoto wake.

Wawili hao walifanikiwa kumpata mtoto huyo mwaka 2007 lakini 2018, walifikishana mahakamani huku mwanamke huyo akidai kufanyiwa mabadiliko ya makubaliano ya mwaka 2011, ambapo Mane alikuwa anatoa dola 2,026.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here