27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Matawi ya Yanga Tabata yanogesha Wiki ya Mwananchi

Nora Damian

Shamrashamra za Wiki ya Mwananchi zimezidi kupamba moto katika maeneo mbalimbali ya nchi ambako kumeshuhudiwa wanachama wa Klabu ya Yanga wakijitokeza kufanya shughuli za kijamii na kutoa misaada ya kibinadamu.

Leo Jumamosi Agosti 3, Umoja wa Matawi ya Yanga Tabata umejitokeza kufanya usafi katika Zahanati za Tabata A na Segerea sambamba na kutoa vifaa vya usafi katika zahanati hizo na mashuka katika Kituo cha watoto yatima cha Malaika kilichopo Kimanga.

Umoja wa Matawi ya Yanga Tabata wakifanya usafi

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa Umoja wa Matawi ya Yanga Tabata, Adeltus Kazinduki, amesema  wameguswa kufanya usafi kuboresha mazingira katika hospitali hizo.

“Wiki ya Mwananchi inamlenga kila raia ambaye yuko katika nchi hii, ndiyo maana kwa umoja wetu tuliamua tuje kufanya usafi hospitalini tuwajali watu wenye mahitaji,” amesema Kazinduki.

Kilele cha Wiki ya Mwananchi kitafikia tamati kesho katika Uwanja wa Taifa ambako Yanga itaivaa Kariobangi Sharks ya Kenya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles