25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

TAWOMA yampongeza Rais Samia ufanisi sekta ya madini

Na Clara Matimo, Mwanza

Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake Tanzania (TAWOMA) kimempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya biashara ikiwemo utulivuwa kisiasa, utawala wa sheria na uendeleza wa miradi mikubwa ya maendeleo ya kitaifa ambayo imefanya shughuli mbalimbali za uzalishaji mali ikiwemo uchimbaji wa madini kuwa na ufanisi.

Wameyasema hayo kwa nyakati tofauti walipozungumza na MTANZANIA DIGITAL jijini Mwanza kwenye viwanja vya Rock City Mall ambako  maadhhimisho na maonesho ya wiki ya madini 2023  yanafanyika kitaifa kwa uratibu wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania(FEMATA).

Baadhi ya wanawake hao wachimbaji  wa madini nchini wamesema uendelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati inayofanywa na Rais Samia ikiwemo ya maji ambayo lengo lake ni kumtua mama ndoo kichwani inawasaidia wanawake kutumia muda ambao wangetafuta maji kufanya shughuli za uzalishaji mali.

Mwenyekiti wa TAHOMA Taifa, Semeni Malale amesema mazingira rafiki ya ufanyaji shughuli za maendeleo yanayowekwa na Rais Dk. Samia ni chachu ya kufikia malengo yao ya kujikwamua kiuchumi wao na taifa kwa ujumla.

Amesema utawala wa sheria na utulivu wa kisiasa unaofanywa na Rais Dk. Samia hapa nchini unaaksi kabisa kauli mbiu ya maadhimisho ya wiki ya madini kitaifa, 2023 isemayo  ‘Amani iliyopo Tanzania Itumike Kuwa Fursa ya Kiuchumi na Tanzania kuwa Kitovu cha Biashara ya Madini Afrika’ kwani bila amani hakuna shughuli zozote za uzalishaji mali zinazoweza kufanyika katika eneo lolote nchini.

“Wanawake ni jeshi kubwa kupitia uongozi wa Rais  wetu Dk. Samia ambao unazingatia utawala wa sheria tunaamini tutafika mbali sana na tutatoa mchango wetu kwa maendeleo ya taifa maana amani anayoilinda ndiyo tunu muhimu sana kwa maendeleo ya taifa,” amesema Malale.

Nae Mwenyekiti wa TAHOMA Mkoa wa Manyara, Fatuma Kikuyu, amesema: “Kwa kweli tunamshukuru sana Rais wetu Dk. Samia kwa kuweka utulivu wa kisiasa sasa tunashirikiana na vyama vyote bila kujali itikadi ya vyama vyetu maana tunachokijali ni kwamba sisi sote ni watanzania na tunahitaji kulijenga taifa letu kwa pamoja.

“Tangu ameingia madarakani hatujasikia matukio ya kutisha yakihusisha watu wasiojulikana, nchi imetulia, ametuunganisha na nchi zingine, hataki dhuluma amesaidia kujenga madarasa, ametutua wanawake ndoo kichwani kweli ni Rais ambaye ni suluhu kama lilivyo jina lake,” amesema Kikuyu na kuongeza:

“Mama Samia amefaa, ametosha na ameweza ametuunganisha watanzania wote bila kujali itikadi za vyama vyetu vya siasa lakini pia tunampongeza sana Waziri wetu wa Madini Dk. Doto Biteko kwa kumsaidia Rais Samia kutuletea maendeleo sisi wananchi wake katika sekta ya uchimbaji,”.

Kwa mujibu wa Kikuyu, Dk. Biteko(Waziri wa Madini Dk. Doto Biteko) amewapa elimu wachimbaji wa mererani kuhusu umuhimu wa kulipa kodi na hasara za kukwepa kulipa kodi ambapo sasa wanaongoza kwa kulipa kodi serikalini kutokana na uzalishaji wanaoufanya.

“Doto ni jembe zamani mererani tulikuwa wakorofi tunakwepa kulipa kodi Biteko amekuja ametufundisha faida za kulipa kodi, hasara za kukwepa kulipa kodi sasa hivi mererani tunaongoza kwa kulipa kodi hakuna anayeiba mawe tena,  kwa kweli Dk. Biteko ni kijana ambaye anaenda na maadili ya kizee,” amepongeza Kikuyu.

Wanawake hao wachimbaji wamesema  kwamba wanaimani na kiongozi wao wa FEMATA Taifa, John Bina kwa jinsi anavyowaunganisha na kushirikiana nao bega kwa bega kutafuta fursa zilizopo katika sekta ya uchimbaji kwa lengo la kuinua uchumi wao na taifa kwa ujumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles