23.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania na Canada kushirikiana katika Sekta ya Madini

NA Mwandishi wetu, Mtanzania Digital

SERIKALI ya Tanzania na Canada zimepanga kushirikiana kwenye maeneo mbalimbali yakihusisha shughuli za utafiti wa madini, kujenga uwezo wa wataalamu na kushirikiana katika kuhamasisha shughuli za uwekezaji nchini ili kuvutia wawekezaji katika Sekta ya Madini.

Hayo yamebainishwa Mei 8 jijini Dar es Salaam na Balozi wa Canada nchini, Kyle Nunas alipokutana na kuzungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Madini,qq1² Kheri Mahimbali na Wataalamu kutoka Wizara na Taasisi katika kikao kilicholenga kuzungumzia shughuli za kuendeleza uchimbaji wa madini.

Akizungumza katika kikao hicho, Katibu Mkuu Mahimbali amesema kuwa, ushirikiano wa Tanzania na Canada katika Sekta ya Madini utaongeza tija kwenye uchumi, kuongeza ajira, kuwajengea uwezo watumishi ili kuwezesha watanzania kuzalisha madini hayo kwa wingi ikiwemo bidhaa zinazotokana na madini hayo.

“Tunaomba tuweze kuwa na ushirikiano na Canada katika kutangaza shughuli za uchimbaji madini zinazofanyika hapa nchini, tuendelee kukutana na kuzungumza mara kwa mara ili mchango wa Sekta ya Madini ukue katika uchumi wetu,” amesema Mahimbali.

Aidha amesema kuwa, Tanzania iko tayari kushirikiana na Cananda kuhakikisha Taifa linanufaika na rasilimali madini ikiwemo madini ya kimkakati ili kukuza uchumi.

Nae Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Dk. Mussa Budeba amesema, ushirikiano wa Cananda kupitia taasisi (Geological Survey of Canada) na Tanzania katika utafiti wa kijiolojia ili kubaini upatikanaji wa madini muhimu na ya kimkakati katika maeneo ambayo hayajafanyiwa utafiti nchiini.

“Ni muhimu sana kubadilishana teknolojia mpya kutoka kwa wenzetu katika utafiti kwa kubadilishana wataalamu kupitia Makubaliano ya mashirikiano (MoU),” amesema Dk. Budeba .

Nae Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini Tume ya Madini Venance Kasiki amemueleza balozi Nunas maeneo ya kusaidia Tanzania katika Sekta ya Madini ni pamoja na kusaidia kujenga uwezo watumishi wa Wizara hiyo kwenye Modeli za Fedha (Financial modeling) na uwezo huo utasaidia katika uchambuzi wa upembuzi yakinifu unaoletwa na wawekezaji kabla ya kutoa leseni za uchimbaji madini.

Tanzania imebarikiwa kuwa na madini mengi ya kimkakati yakihusisha madini ya nikeli, kinywe, rare earth elements, cobalt, chuma na madinini mengine ambayo ndiyo yanahitajika kwa sasa duniani kwa ajili ya kutumika katika teknolojia mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles