27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Tausi: Nitaibua, kukuza vipaji vya wanamitindo

TausiNA SALMA MPELI, DAR ES SALAAM
MWANAMITINDO wa Tanzania ambaye anafanya shughuli zake nchini Marekani, Tausi Likokola, amepania kuibua na kukuza vipaji vya wanamitindo wachanga.
Akizungumza katika Ofisi za New Habari (2006) LTD hivi karibuni, Tausi alisema kwa kuona umuhimu wa kuibua vipaji vya wanamitindo ameamua kufungua studio yake binafsi ambayo itakuwa ikitoa mafunzo mbalimbali ya urembo.
“Tanzania tuna vipaji vingi tatizo hakuna watu wa kuviangalia na kusimamia, ndiyo maana nimeamua kuisaidia nchi yangu kuvumbua wanamitindo wapya,” alisema Tausi.
“Wiki mbili zilizopita nilikuwa na Flavian Matata, tunafanya vizuri sana kwa sasa, nafurahi kuona akiipeperusha vyema bendera yetu,” alisema Tausi.
Tausi ambaye amekuwa akifanya shuguli zake za urembo nchini Marekani, amepania kuendelea kuitangaza Tanzania zaidi kupitia sekta hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles