Albamu mpya ya Barnaba kuandaliwa miezi mitatu

0
1194

barnabaNA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Barnaba Elias ‘Barnaba Classic’, amesema atatumia muda wa miezi mitatu kundaa albamu yake mpya.
Akizungumza jijini hivi karibuni, Barnaba alisema matarajio yake ni kuingiza sokoni albamu hiyo kabla ya kumalizika kwa mwaka huu.
“Unajua tangu nilipoachia ile albamu ya kwanza imepita miaka miwili, nadhani ni muda mwafaka wa kuandaa kitu kingine kwa mashabiki zangu,” alisema Barnaba.
Barnaba alisema shuguli ya kuandaa albamu hiyo ilianza juzi, ambapo atakuwa anatumia muda mwingi kukaa studio kuandika mistari na kurekodi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here