28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Timbwili laibuka mkutano Simba

simbaNA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM

MKUTANO mkuu wa dharura wa klabu ya Simba ulifanyika jana kwenye Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam, huku ukiibua timbwili baada ya baadhi ya wanachama kutoleana lugha chafu.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wanachama 514, lakini sehemu kubwa ya viti ilionekana kuwa tupu tofauti na ilivyotarajiwa, huku ukihusisha ajenda tatu, ya kwanza ambayo ni kubwa ilihusu kujadili mwenendo wa mbaya wa Simba kwenye Ligi Kuu ya Vodacom.

Ajenda ya pili ilikuwa ni ya mradi wa Uwanja wa Simba uliopo Bunju, Dar es Salaam, huku ya tatu ikijadili wanachama wapya na kadi za wanachama, ajenda zote hizo zilitambulishwa na Rais wa timu hiyo, Evans Aveva.

Timbwili hilo lilianza wakati wanachama wa klabu hiyo waliporuhusiwa kutoa maoni yao kuhusu ajenda ya kwanza ya mwenendo wa Simba, iliyokuwa imemalizwa kuelezewa na Aveva.

Aliyeanzisha timbwili hilo ni Katibu Mkuu wa Tawi la Ngome Kongwe la klabu hiyo lililopo Tabata, Karim Tamim, aliyeinuka kwenye kiti na kuanza kumshambulia kwa maneno mchangiaji wa kwanza, Ramadhan Don King, ambaye ni Mwenyekiti wa matawi ya Simba.

Tamim alimjia juu Don King baada ya kuunga mkono maelezo ya Aveva juu ya sababu za kuboronga Simba, huku akishindwa kujadili hoja na kubaki kuusifia uongozi wake, pia baadhi ya wanachama wengine nao walianza kumfokea.

Baada ya kutokea zogo hilo miongoni mwa wanachama, Aveva aliwatuliza na hali kuwa shwari ukumbini hapo na wanachama wengine kuendelea kutoa maoni yao.

Lakini katika hali kushangaza, kuna baadhi ya wanachama walishindwa kutoa maoni yao, licha ya kunyoosha vidole kwa muda mrefu ili wachaguliwe kuzungumza, huku minong’ono ikiibuka kuwa kuna baadhi ya watu waliandaliwa kuzungumza.

Ufuatao ni mchanganuo wa ajenda zote tatu zilizojadiliwa;

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles