27.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

TAUSI LIKOKOLA CHACHU YA MAFANIKIO KWA WANAWAKE

Na AGATHA CHARLES


“SIKU ya wanawake duniani inapaswa kusherehekewa kila siku, isiwe kwa siku maalumu kutokana na umuhimu na mchango mkubwa wa wanawake kwa jamii…wanawake wanapaswa kupendwa, kulindwa na kuheshimiwa.” Hii ni kauli ya Tausi Likokola.

Tausi ni mwanamke nyota wa mitindo pia ni kielelezo cha nembo ya urembo kitaifa na kimataifa.

Katika dunia ya sasa suala la mitindo lina nafasi kubwa katika uwakilishi wa mataifa mbalimbali pia linatoa fursa katika kujikwamua kiuchumi. Tausi Likokola anang’ara kimitindo na amekuwa chachu ya mafanikio ya wanawake wengi wanaochipukia katika tasnia ya mitindo nchini.

Katika siku hii ya wanawake duniani ambayo inaadhimishwa leo, Tausi anaelezea wajibu wa wanawake na umuhimu katika ngazi ya kifamilia na Taifa kwa ujumla.

“Wanawake ni mama, wafanyabiashara, madaktari, wanasheria, walimu, wasanii, wabunifu, mama wa nyumbani,” anasema Tausi.

Tausi ambaye aling’ara katika anga la mitindo kimataifa kwa zaidi ya miaka 20, anasema; “Kila siku mwanamke anapaswa kujiangalia vyema kwenye kioo na kusema ‘nakupenda’ unafanya kazi nzuri. Mtangulize Mungu, kuwa nyota, kuwa wa mfano na pambana,” anasema Tausi.

Katika kuenzi alichonacho ili kiwasaidie wanawake wengine, alijikita kutoa elimu ya urembo na mitindo kupitia kipindi chake cha Televisheni cha Tausi Likokola’s African Princess Model Search.

Anasema kipindi hicho ni mchanganyiko wa vitabu vyake Beautiful you na African Princess ambacho kinatoa uhalisia wa mitindo kwa kutoa elimu, kuongoza, kujiamini, kujituma n.k.

“Ukiangalia kipindi changu, si tu kwa mwanamitindo, msichana yeyote anaweza akaangalia na kujifunza jinsi ya kutengeneza ngozi yake au jinsi ya kujisukuma katika maendeleo,” anasema Tausi.

Tausi pia ni mwanamke mjasiliamali anayetengeneza nywele ziitwazo Tausi Beautiful you Hair pamoja na perfume (manukato) inayoitwa Tausi Dreams.

Anasema Tausi Beautif you Hair ni nywele halisi (Human hair) ambazo alianza kuzitengeneza huko Las Vergas, nchini Marekani na hivi sasa anazitengenezea nchini China.

Katika uandishi, Tausi ana vitabu vinne The African Princess, ‘Beautiful You’, ‘The Art of Beauty & Health’ na ‘The touch of an Angel’ ambavyo alianza kuviandika na kuvitoa miaka nane iliyopita.

 

Soko

“Soko bado ni gumu, watu wanaona ni bora wanunue kitu cha bei rahisi kuliko kuwekeza kununua kitu kizuri, kuna soko nililokuwa nimelilenga, wateja wanakuja lakini hawajafikia kiasi ambacho naweza kusema bidhaa imetoka kwa wingi,” anasema Tausi.

Tausi ambaye miaka ya nyuma alifanya mitindo kimataifa kupitia kampuni kubwa kama Gucci, Christian Dior, Issey Miyake, Tommy Hilfger, Escada n.k miradi yake anaifanya kupitia kampuni zake mbili za ‘Tausi and Friends for Life’ na ‘Tausi Dreams Ltd’

 

Urembo

Tausi kama mama wa watoto wawili bado anaoenekana ni msichana. Mwenyewe anasema siri kubwa ya mwonekano wake ni kunywa maji mengi, mbogamboga na kufanya mazoezi.

“Natumia losheni za kawaida za Nivea na bidhaa zenye Alovera, nakunywa maji ya kutosha, nakula zaidi mboga za majani, samaki na kuku kuliko bidhaa za kusindika pamoja na nyama nyekundu.

“Pia nafanya ‘routines’ za mazoezi nyumbani ambavyo vyote vinasaidia ngozi nzuri na mwili mzuri,” anasema Tausi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles