30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

SERIKALI KUMLINDA MMILIKI EFM

 

NA EVANS MAGEGE

-DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ameahidi kulinda uwekezaji wa mmiliki wa kituo cha Redio EFM na Tv E, Francis Ciza (Majizo) na kumtaka kutotishwa na kelele za barabarani.

Nape alitoa kauli hiyo jana wakati alipotembelea makao makuu ya kituo hicho cha redio hiyo, Kawe jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa akiwa waziri mwenye dhamana ya habari ana wajibu wa kulinda habari pamoja na wawekezaji katika tasnia nzima ya habari na kuwataka wafanyakazi wa kituo hicho kutokuwa na hofu kwani kazi wanayoifanya ina baraka za Mungu.

“Kama serikali na kama waziri mwenye dhamana ya habari nimeshuhudia kwa macho yangu uwekezaji uliouweka hapa, tutalinda uwekezaji uliouweka usiharibiwe ovyo… Si Watanzania wengi wenye maono haya, najua umeanza mbali hadi kufika hapa, si kazi rahisi ndiyo maana nasema ukiona mtu kasimama si vizuri kwenda kumparamia ovyo.

“Ni vizuri kuheshimu kazi ambayo amehangaika nayo, jasho si la bure, uwekezaji huu ni mkubwa sana labda iwe hujui alichowekeza, hujui kapambana kiasi gani kufika hapo ndiyo unaweza kufanya unachotaka, kwa mtu yeyote mwenye mapenzi mema na Dar es Salaam  na Tanzania kwa ujumla atawalindeni na kuhakikisha mnapata ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yenu,” amesema Nape.

Awali kabla ya Nape kutoa hotuba yake, Meneja Mkuu wa redio EFM/ Tv-E, Dennis Sebbo alisema katika kuhakikisha redio hiyo inaendelea kutimiza malengo yake, imeamua kuongeza masafa na kusikika nchi nzima ambapo kwa sasa wataanza katika mikoa tisa ikiwamo Mwanza, Mbeya, Mtwara, Tanga, Manyara, Singida, Kigoma, Tabora na Kilimanjaro.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles