24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

TATTOO ZA MASTAA ZILIZOFUTWA BAADA YA MAPENZI KUVUNJIKA

NA CHRISTOPHER MSEKEN


MICHORO ya mwilini inayofahamika kama ‘Tattoo’ imekuwa ikitumiwa na watu mbalimbali katika kuhifadhi kumbukumbu ya vitu ambavyo mchorwaji anakuwa amavidhamiria kuviweka kwenye mwili wake.

Tattoo inaweza kuchorwa kama urembo, kumbukumbu  au alama ya kitu fulani ambacho kinakuwa na umuhimu kwa mtu aliyechora ndiyo maana tunaona wapendanao wengi wakichorana michoro hiyo kama alama ya inayoonyesha upendo wao.

Bongo pia tumeendelea kushuhudia mastaa mbalimbali wakionyeshana ubabe wa kupendeza kwa kuchora tattoo zenye maana tofauti huku kapo kadhaa za mastaa nazo zikichorana michoro hiyo iliyoanza kuchworwa kitamaduni nchini Japani mnano karne ya 18.

Juma3tata leo tunakuletea orodha ya mastaa wa Bongo ambao walipagawa na mapenzi kiasi cha kuchora tattoo za wapenzi wao na baadaye kuzifuta baada ya kapo zao kuvunjika.

Amber Lulu & Young Dee

Julai 20 mwaka huu, ilifahamika kuwa Amber Lulu ameifuta tattoo yenye jina la Young Dee katika mkono wake na kubadilisha mchoro. Wawili hao wote wawili wamewahi kukanusha kuwa wapenzi japo kuwa Young Dee amewahi kunukuliwa akisema yeye na Amber Lulu waliwaahi kudondoka kitandani.

Shilole & Nuh Mziwanda

Shilole hivi sasa ameposwa na jamaa anayeitwa Asharafu Uchebe na ndoa yao inatarajia kutikisa nchi ifikapo Desemba 20 mwaka huu, siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mrembo huyo.

Lakini Shilole enzi za ujana wake kwenye tasnia ya mapenzi aliwahi kuwa na uhusiano na msanii, Nuh Mziwanda, penzi lao lilikuwa maarufu mno kutokana na matukio waliyokuwa wanayafanya pamoja.

Desemba 30 mwaka 2015 ilifahamika kuwa Shilole aliifuta tattoo yenye jina la Nuh Mziwanda aliyoichora katikati ya maziwa yake, aliibadili na ikawa kama ua fulani hivi nzuri nzuri.

Hali kadharika Februari 7 mwaka 2016, Nuh naye aliifuta tattoo ya Shilole iliyokuwa kwenye mkono wa kushoto ikisomeka Shishi Baby, alifanya hivyo baada ya penzi lao kuvunjika.

Nawal

Huyu ni mzazi mweza wa Nuh Mziwanda. Wawili hawa walifunga ndoa kamili ya Kiislamu, Novemba 10 mwaka jana na kufanikiwa kupata  mtoto mmoja anayeitwa Anyagile.

Mwaka huu ndoa hiyo ilivunjika baada ya Nuh kurudi kwenye dini yake ya Kikristo ambapo enzi wapo pamoja, Nawal alijichora Tattoo yenye jina la Nuh Mziwanda ambayo hivi sasa ameibadilisha na imekuwa kama mchoro wa ua.

Fahamu

Kuwa hao ndiyo mastaa ambao walifuta Tattoo za wapenzi wao baada ya kapo zao kuvunjika lakini pia nikujuze kuwa msanii Harmonize naye aliwahi kufuta tattoo yenye sura ya bosi wake (Diamond Platnumz,) kisha kuichora tena nyingine nzuri kwenye mkono ikiwa chini ya tattoo nyingine yenye sura ya mama yake mzazi, hiyo ilikuwa mwaka jana mwezi Agosti.

Kwa maoni, ushauri na pongezi zako tuma meseji kwenye namba 0756 074 048.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles