24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

PETER: SIHUSIKI P-SQUARE KUVUNJIKA

LAGOS, NIGERIA


NYOTA wa muziki nchini Nigeria ambaye alikuwa anaunda kundi la P-Square, Peter Okoye, ameweka wazi kuwa yeye si chanzo cha kundi hilo kuvunjika.

Kundi hilo kwa sasa limevunjika kwa madai kwamba kila mmoja alikuwa anafanya mambo kinyume na utaratibu na kila mmoja sasa anafanya kazi peke yake.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, mapacha hao walikuwa wanasherehekea siku yao ya kuzaliwa, lakini kila mmoja alionesha kusherehekea kivyake japokuwa Paul aliposti picha yao ya utotoni.

Taarifa zilisambaa kwenye mitandao kwamba Peter ndio chanzo cha kuvunjika kwa kundi hilo, lakini ametumia ukurasa wake wa Instagram na kukanusha taarifa hiyo.

“Nashangaa kuonekana kuwa mimi ndio mwenye kosa, hakuna ukweli wowote nadhani kosa langu ni kuweka wazi tofauti zetu, ila mimi si chanzo kama watu wanavyosema kwenye mitandao ya kijamii, lakini nashukuru kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa,” aliandika Peter.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles