26.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

SELENA AFUTA PICHA ZA THE WEEKND

NEW YORK, MAREKANI


NYOTA wa muziki na filamu nchini Marekani, Selena Gomez, amezidi kuthibitisha kuwa ameachana na mpenzi wake, The Weeknd, baada ya juzi kuamua kuzifuta picha zake kwenye akaunti ya Instagram.

Selena alikuwa anatoka na rapa huyo kwa muda mrefu mara baada ya kuchana na Justin Bieber, lakini taarifa zilizopo mitaani ni kwamba mrembo huyo ameachana na The Weeknd na kuamua kurudi kwa Bieber.

Selena ameamua kufuta picha za rapa huyo kwenye akaunti yake pamoja na ‘kumuunfollowed’, hivyo mashabiki tayari wanaamini kuwa wawili hao wameachana na mrembo huyo ameamua kurudi kwa mkali anayetamba na wimbo wa ‘Sorry pamoja na Love Your Self’.

Hata hivyo, mbali na Selena kuachana na rapa huyo na kumfuta kwenye akaunti zake, lakini bado hajamfuata Bieber kwenye akaunti zake za kijamii kama ilivyo awali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles