25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

NI WAPI CECAFA WANAPOKOSEA? (1)

Na WAANDISHI WETU -DAR ES SALAAM


MASHINDANO ya soka kwa nchi za Afrika mashariki na Kati maarufu kama CECAFA yalianzishwa mwaka 1927. Ni mashindano makongwe mno ya kikanda kuliko mengine kama ya WAFU au COSAFA. Shirikisho hilo limekuwa kikiendesha mashindano ya Chalenji kwa timu za Taifa, Klabu, Nile Basin na mengine chini ya miaka 17 na 20 kwa wanachama wake.

Wanachama wa CECAFA kwa sasa ni Burundi, Djibouti , Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda , Somalia, Somalia, Sudan kusini, Sudan, Tanzania, Uganda na Zanzibar. Pamoja na ukongwe wa mashindano hayo yamekuwa yakifanyika kwa kusuasua. Ni amshindano ambayo yana historia ya muda mrefu lakini kila yanapitakiwa kufanyika yamekuwa yakikosa muda sahihi kama ilivyo kwa mashindano ya WAFU kwa nchi za Afrika magharibi.

WAFU

Kwa mfano, mashindano ya  WAFU ya mwaka huu yameshirikisha imu 16 ikiwa ni kiwango cha juu zaidi tangu yaliporudishwa tena mwaka 2002. Awali mashindano hayo yalikuwa yanashirikisha timu 8 tu kabla ya kufanya mabadiliko makubwa ya kiuendeshaji yaliyovutia wadhamini na washiriki. Hadi mwaka 2013 ni timu 8 pekee zilishiriki mashindano hayo yaliyofanyika nchini Ghana na mwenyeji kuibuka bingwa.

Mashindano ya WAFU yalianzishwa mwaka 1974, lakini yalisimamishwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo hali mbaya ya usalama kwa nchi wanachama wa Afrika magharibi. Lakini mwaka 2002 yalirejeshwa kabla ya kufungwa tena. Kuanzia mwaka 2010 mashindano hayo yamekuwa imara zaidi ambapo wadhamini wanapigana vikumbo kutoa ofa. Mwaka 2017 mashindano hayo yalifanyika mwezi Julai, ambapo yalidhaminiwa na Kituo kikubwa cha Televisheni cha Fox Sports kutoka nchini Marekani. Kituo hicho kinaonyesha mashindano hayo katika nchi mbalimbali kuanzia afrika masgharibi yenyewe, afrika mashariki, kusini mwa afrika, Marekani na maeneo mengine. Ikiwa na maana manufaa ya mashindano ya WAFU ni makubwa kuliko ya CECAFA. Aidha, mashindano ya WAFU hayakupata utaratibu kamili wa muda wa kufanyika. Kwa mfano mwaka 2010 na 2011 yalifanyika Nigeria. Mwaka 2013 na 2017 yamefanyika nchini Ghana. Hivyo utabaini kuwa uenyeji wa Nigeria ulikuwa wa mfululizo wakati Ghana imeandaa kukiwa na tofauti ya miaka mitatu.

COSAFA

Mashindano haya yanashirikisha timu 14 ambzo hupangwa katika makundi mawili ya timu 8. Mshiriki wa 14 huwa anaalikw akama ilivyopewa nafasi Tanzania kwa mwaka huu. wanachama wa COSAFA ni Angola, Madagascar, Malawi,Mauritius, Mozambique, Shelisheli, Zimbabwe, Botswana, Lesotho, Namibia,m Afrika kusini, Swaziland na Zambia. Mashindano haya huonyeshwa moja wka moja na televisheni ya Supersport ambayo inayo haki ya kurusha matangazo yake kusini mwa bara la afrika pamoja na afrika mashariki na kati. Kama ilivyo kwenye mashindano ya COSAFA, Supersport pia inayo haki ya kurusha matangazo ya CECAFA katika nchi za kusini mwa afrika na afrika mashariki.

UONGOZI

Tofauti ya uendeshaji w amashindano hayo ni uongozi wenye nia thabiti na malengo ya kufika mbali. WAFU wamefanikiwa kuwashawishi Fox Sports kurusha mashindano yao, wakati CECAFA ambayo ni mashindano makongwe yamebaki kujikongoja tu. COSAFA ni mashindano ya uhakika, licha ya kupitia kwa wadhamini tofauti wakiwemo Castle Lager ambapo mwaka 2015 wlaiingia mkataba wa miaka mitano kuendesha mashindano hayo. Hali hiyo ni tofauti na CECAFA ambako suala la wadhamini limekuwa tatizo kubwa na chanzo cha kushindwa kufanyika mashindano hayo.

Maahindano ya WAFU yamezivutia timu hadi sasa zimefika 16 ikiwa na maana kushindwa kwa CECAFA kunatokana na amsuala ya uongozi ndani ya shirikisho hilo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles