26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

TAS: Wenye Ualbino wanakaidi kuvaa kofia

Na Derick Milton, Simiyu

Chama cha Watu wenye Ualbino (TAS) Mkoa wa Simiyu kimeiomba Serikali kutunga Sheria ambayo itawalazimisha watu wenye Ualbino kuvaa kofia maalumu za kuzuia mionzi ya jua pamoja na nguo ndefu kwa ajili ya kulinda ngozi ya miili zao.

Katibu wa Chama hicho, Juma John ametoa ombi hilo kwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu, Ummy Nderiananga, wakati wa kikao na makundi ya watu wenye ulemavu mkoani humo.

John amesema kuwa baadhi ya watu wenye Ualbino wamekuwa wakikaidi kutumia vifaa hivyo licha ya kuwa navyo na wamepewa bure na serikali na wengine kupewa na wadau mbalimbali.

Amesema kuwa Chama hicho kimekuwa kikikutana na watu wao ambao wanawajua kuwa wanavyo vifaa hivyo, lakini hawavitumii na wanakutwa wamevaa kofia za kawaida ndogo pamoja na nguo fupi.

“Tunaomba serikali kama kuna uwezekano itungwe sheria kama kutulazimisha watu wenye ualbino, baadhi yetu wanakaidi kuvaa kofia zile kubwa maalumu na nguo ndefu.

“Tunakutana na watu uko njiani wamevaa nguo fupi tena za mikono mifupi, kifua wazi na hazifiki chini, hiyo ni hatari sana, lakini mavazi maalumu wanayotakiwa kuvaa wanayo ila hawataki, ni vyema ikatungwa sheria ya kulazimisha,” ameeleza John.

Akiongea katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga, ameunga mkono ombi la watu wenye ualbino, ambapo ameeleza kutokuvaa nguo hizo na kofia maalumu ni kosa la jinai.

“Ni kweli kama mtu mavazi yote anayo na anakaidi tunaweza kusema ni kosa la jinai (anataka kujiua), ni vyema sheria ikawepo kwa ajili ya kuwalinda,” amesema Kiswaga.

Akifunga Mkutano huo Naibu Waziri huyo amewataka watu wenye Ualbino kuhakikisha wanatumia mavazi maalumu waliyonayo na wanayotakiwa kuvaa wakati wa joto.

“Ni kweli kama mtu mavazi yote anayo na anakaidi tunaweza kusema ni kosa la jinai (anataka kujiua), ni vyema sheria ikawepo kwa ajili ya kuwalinda,” amesema Kiswaga.

Aidha, Ummy amewataka waganga wafadhiwi wa hospitali na vituo vya Afya nchini kuhakikisha wananunua mafuta maalumu kwa ajili ya watu wenye ualbino kwani sasa hivi yanapatikana bohari kuu ya dawa (MSD).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles