Na Sheila Katikula, Mwanza
Serikali imeobwa kutupia macho kwenye shule binafsi ambazo zinawaondoa wanafunzi wenye uwezo mdogo darasani wanaotarajia kuingia kwenye madarasa ya mitihani ya kitaifa.Â
Rai hiyo imetolewa na Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Thaqaafa, Zena Opiyo alipokuwa akizungumza kwenye mahojiano maalum na mwandishi wa habari ofisini kwake.Â
Alisema kuna baadhi ya shule zimejiwekea wastani mkubwa wa ufaulu tofauti na uliowekwa na serikali kwa lengo la kuwaondoa wanafunzi wenye uwezo mdogo ili shule zao zisipate daraja la nne na sifuli.Â
“Inasikitisha kuona baadhi ya wamiliki wa Shule hupanga wastani wao tofauti na uliopagwa na serikali hasa kidato cha pili na wakiona mwanafunzi amefaulu wastani wa taifa na hajafilisha waliopanga wao huwafukuza kwa madai hana vigezo vya kusoma hapo,”alisema Opiyo.Â
Naye Meneja wa Shule za Alliance zilizopo jijini hapa, James Bwire alisema ushindani wa biashara husababisha viongozi wa shule kupendelea kubakia na wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye mitihani.