28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Tarura yazidai halmashauri Sh milioni 130.

Na Derick Milton, Simiyu.

Wakala wa Barabara mjini na Vijijini (Tarura) Mkoa wa Simiyu, imeuomba uongozi wa Mkoa huo kusaidia kupata fedha zake ambazo wanazidai halmashuari ya wilaya ya Meatu pamoja na Bariadi vijijini.

Ombi hilo limetolewa leo na Mratibu wa wakala huo Mkoa, Mhandisi Dk Philimoni Msomba, wakati wa kikao cha bodi ya barabara mkoa, ambapo amesema wanazidai halmashuari hizo zaidi ya Sh milioni 134.

Msomba amesema kuwa katika halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Tarura inadai zaidi ya Sh milioni 97.5 huku Bariadi Vijijini wakidai zaidi ya Sh milioni 37.1, fedha ambazo amesema wamezidai toka mwaka 2017.

“Halmashauri hizi zilitumia fedha hizi kutoka mfuko wa barabara, baada ya tarura kuanzishwa tulikuta tayari wamezitumia, tukaendelea kuwadai lakini mpaka leo bado hawajazirejesha, tunaomba viongozi wa mkoa, mtusaidia tupate fedha hizi ili tuwalipe wanaotudai,” amesema Msomba.

Katika kikao hicho Mratibu huyo amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2020/21, Tarura imepanga kutumia Sh bilioni 5.1 kwa ajili ya ukarabati wa madaraja pamoja na barabara kilometa 822.

Hata hivyo mratibu huyo amewaomba wabunge wa mkoa huo, kutumia nafasi yao kuipigania Tarura ili iweze kuongezewa mgao wa fedha kutoka mfuko wa barabara kwani kwa sasa wanapatiwa asilimia 30 huku Tanroads wakipata asilimia 70.

Naye Meneja wa Wakala wa Barabara mkoa (Tanrods), Albert Kent akiwasilisha makisio ya bajeti ya mwaka 2020/21, amesema kuwa wamepanga kutumia Sh bilioni 11.4 kwa ajili ya matengenezo ya barabara kilometa 900 yakiwemo na madaraja.

Kwa upande wao wajumbe wa kikao hicho wakiwemo wabunge, wameiomba serikali kuiongezea bajeti Tarura kwani kiasi cha fedha ambacha wanapewa kwa sasa ni kidogo sana kulinganisha na mtandao wa barabara walionao ambao ni mkubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles