31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Baraza la madiwani Moshi Vijijini kujadili changamoto za walemavu

Na Safina Sarwatt, Moshi,

Naibu Waziri wa Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu wenye Ulemavu, Ummy Nderiananga ameigiza baraza la madiwani Halmashauri ya wilaya Moshi vijijini kuweka utaribu wa kujadili masuala yanayowahusu watu wenye ulemavu ili kutatua changamoto zinazowakabili makundi hayo.

Ndeliananga ameyasema hayo leo Desemba 15, katika kikao cha Baraza la Halmashauri hiyo wakati wakuapisha madiwani pamoja na uchaguzi wa mwenyekiti wa halmashauri na makamu mwenyekiti.

Waziri Ndeliananga amesema makundi hayo ya watu wenyewe ulemavu wana mchango mkubwa katika taifa haswa katika hicho ambacho nchi imeingia uchumi wa kati.

“Kuna haja ya kuwapa viapumbele watu wenye ulemavu, hivyo ni vema halmashauri ikatengeneza programu ya kujadili masula ya watu wenyewe ulemavu kwani ni moja ya kundi ambalo linamchango mkubwa katika ustawi wa uchumi wa taifa.

“Tuone namna yakuweza kuwasaidia makundi haya tunapoelekea katika uchumi wa kati ni namna gani wamechagia katika ukuaji wa uchumi wa taifa hili,” ameongeza

Katika uchaguzi huo wa mwenyekiti wa baraza la madiwani halmashauri ya wilaya Moshi Moris Makoi alipata kura 46 na Makumu Mwenyekiti, Filberth Shayo kura 47.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles