25.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

TARI yagundua mchicha unaoongeza nguvu za kiume

Safina Sarwatt, Arusha

Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI-Tengeru) imegundua kugundua mchicha lishe wa akeri ambao unaelezwa kuwa na madini Zinki huku pia ukiimarisha nguvu za kiume kwa wanaume wenye changamoto hiyo.

Tari inasema kuwa changamoto ya upungufu wa damu, udumavu pamoja na uoni hafifu kwa watoto na wajawazito nchini linakwenda kumalizika baada ya kugundulika kwa mchicha huo.

Kwa mujibu wa tafiti zilizofanyiwa na taasisi hiyo mchicha huo kugundulika kuwa unaprotini asilimia 14.5 huku ukiwa ni chanzo bora cha vitamini A, B, Zinki, madini ya chokaa, chumvi na folikasidi.

Akizungumza hivi karibuni jijini Arusha katika ziara ya Mafunzo ya Waandishi wa Habari kutoka Kanda ya Kaskazini iliyoratibiwa Tume ya Taifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu (COSTECH), Mtafiti Mwandamizi, Emmanuel Lasway kutoka TARI Tengeru amesema utafiti umebaini mchicha huo unakwenda kupunguza tatizo la upungufu wa damu pamoja udumavu endapo utatumiwa vizuri.

Amesema kuwa endapo matumizi ya mchicha huo yatazingatiwa na wajawazito, watoto na wanaume ambao wanakabiliwa na tatizo la nguvu za kiume itasaidia kumaliza changamoto hiyo na kuondokana na hali hiyo.

“Kwa wanaume tunawashauri kutumia nafaka ya mchicha wa akeri kutokana na namna ambavyo umefanyiwa utafiti wa kina na kubainika kusaidia kupunguza tatizo nguvu za kiume.

“Hivyo kwa wanaume wenye changamoto hiyo wataweza kuimarisha ndoa zao na kuboresha mfumo wa uzazi,” amesema Lasway.

Kwa mujibu wa mtafiti huyo mchicha huo wa maajabu huvunwa shambani na kisha mbegu zake husagwa na kuchanganya kwenye vyakula ili kuongeza virutubisho.

Aidha, ameongeza kuwa mchicha huo pia una lishe unachangia kiasi cha asilimia 50 hadi 102 ya folikasidi ukilinganisha na mahindi asilimia 15-46 na ngano asilimia 20 hadi 51.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles