24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Wakulima nchini washauriwa kutumia maabara ya TARI-Tengeru

Na Safina Sarwatt, Arusha

Wakulima nchini wameshauriwa kuitumia maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania Kituo cha TARI TENGERU iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha ili waweze kutambua magonjwa na kupata ushauri wa watalamu wa kilimo na Uthibiti wa magonjwa na visumbufu vya mimea.

Akizungumza hivi karibuni wakati ziara ya mafunzo ya Wandishi wa Habari kutoka mikoa ya Kanda ya Kaskazini yaliyoratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifuni COSTECH Msimamizi na Mratibu wa mradi wa Maboresho ya Maabara hiyo, Mtafiti Dk. Fatuma Kiruwa amesema kituo hicho kimeendelea kufanya vizuri katika tafiti za magonjwa ya mimea pamoja na uzalishaji wa miche bora ya migomba ambayo haishambuliwi.

Amesema kuwa wakulima wengi bado hawana uelewa kuhusu huduma za utafiti hasa magonjwa ya mimea hali inayowapelekea kushindwa kuzalisha kwa tija.

“Ushauri wangu kwa wakulima kwamba watumie fursa zilizopo za maabara hii kufuatilia utaalamu kutoka kwa watafiti wa kilimo pamoja na maafisa ugani ili waweze kuzalisha kwa tija badala ya mkulima kukimbilia dukani na kutumia kemikali bila kushauriwa na wataalamu hao,” amesema.

Amefafanua zaidi kuwa lengo la kuanzishwa kwa maabara nikutoa huduma bora na kufikia wakulima wengi ili waweze kutumia matokeo ya tafiti zilizofanywa katika kuzalisha miche bora migomba ambayo hazishambuliwa wadudu, pamoja na vipando vya mimea .

Amesema mpaka hivi sasa miche ambayo tayari imeshafanyiwa tafiti na kuleta matokeo mazuri ni migomba,mchicha na maparachichi aina HASI hususani kipindi chote cha kilimo na tumefanikiwa kumuinua mkulima kiuchumi na kufikia malengo yake.

Amesema miche inayotoka kwenye maabara hiyo inakuwa na uhakika wa usafi na kutokuwa na magonjwa na wadudu hivyo mkulima anapokwenda kupanda shambani wanauhakika wa mbegu anayoipanda na itatoa mazao ya uhakika kwa muda unaohitajika na kumwezesha mkulima kushindana katika soko hususan soko la ndani na nje ya nchi.

Nae Mtafiti Mwandamizi TARI TENGERU, Emmanuel Mlinga amewakaribisha wakulima kufika katika Taasisi hiyo kujionea Miche mbalimbali iliyothibitishwa kiutafiti ikiwemo ile ya parachichi na pia waweze kushirikiana na watafiti wabobezi kujibu kero zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles