28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Tarehe ya hukumu dhidi ya kesi inayomkabili Rais Museveni yatangazwa

Kampala, Uganda

Jopo la majaji tisa wa Mahakama ya juu nchini Uganda wametangaza kuwa Machi 18, mwaka huu ndiyo watatoa hukumu ya kesi iliyowasilishwa na Robert Kyagulanyi kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais yaliyompatia Museveni ushindi.

Majaji hao kwa mara ya kwanza wamekutana na pande zote mbili katika mahakama hiyo mjini Kampala na kutoa muongozo wa kuanza kusikiliza kesi kwa muda wa siku 45 zinazotakiwa na katiba ya Uganda.

Jaji Mkuu wa Uganda, Alfonse Dollo, ndiye ameongoza jopo la majaji wanaosikiliza kesi hiyo ya Robert Kyagulanyi.

Jaji Mkuu amezitaka pande zote mbili kuzingatia muda waliopewa kwa kutoa ushaidi, kwani hukumu ya kesi imepangwa kutolewa Machi 18.

Kyagulanyi kupitia kwa mawakili wake wanamshtaki Rais Museveni, Tume ya uchaguzi na mwanasheria mkuu, ambao wote walikuwepo mahakamani kutetea ushindi wa Rais Museveni aliopata wa asilimia 58.

Kuanzia leo upande wa mashtaka na washitakiwa watakuwa wanabadilishana nyaraka za kesi hiyo na mashaidi hadi Machi 5, ameeleza Asumani Basalirwa, wakili wa Bobi Wine.

Hii ni mara ya nne kwa Rais Yoweri Museveni kushitakiwa na wapinzani wake baada ya kutangazwa mshindi, Dk. Kiiza Besigye, alimshitaki mara mbili na Amama Mbabazi mwaka 2016 lakini Rais Museveni aliibuka mshindi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles