23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama ya kijeshi yahukumu raia kifungo cha miaka 100 Uganda

Kampala, Uganda

Mahakama ya Wilaya huko Mbarara imewahukumu raia wawili kifungo cha miaka 100 gerezani kwa kosa la kumuua Afisa wa polisi na kukimbia na silaha yake katika wilaya ya Kabale.

Wawili hao; Mukwenda Mugisha(19), mkazi wa kijiji cha Gatete na Paul Dusingizimana(27) mkazi wa Manispaa ya Kabale walipatiwa hukumu hiyo siku ya Alhamisi, Gazeti la Daily Monitor la Uganda limeripoti.

Mashtaka yakingozwa na Luteni James Omondi yaliyowasilishwa Januari 24, yamesema Mugisha na Dusingizimana walimshambulia na kumuua, Gracious Byaryabakabu, aliyekuwa zamu ya kulinda Ofisi ya Tume ya Uchaguzi ya Wilaya ya Kabale. Walimpora silaha yake iliyokuwa na risasi takribani 30.

”Watuhumiwa hao pia walimpora Godfrey Tukamubona simu yake ya mkononi yenye thamani ya Sh za Uganda 60,000 baada ya kumsababishia madhara makubwa,” alisema

Mahakama pia ilielezwa kwamba mnamo Januari 29, wakiwa katika gereza la Rutenga katika Manispaa ya Kabale, wawili hao walimtisha, Patrick Arinaitwe kwa bunduki, walimteka nyara na kumuibia Sh 20,000 zilizokuwa kwenye akaunti ya simu ya mkononi

Watuhumiwa walikutwa na hatia ya makosa yote matatu ya unyang’anyi, mauaji na utekaji nyara.

Hata hivyo wawili hao wameomba huruma ya mahakama ya kuwapunguzia adhabu kwani walikuwa ”wamelewa ” walipokuwa wakitekeleza vitendo hivyo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles