New York, Marekani
Wajumbe wa nchi wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) wanakutana mjini New York baadaye leoFebruari 12, kumchagua Mwendesha Mashtaka mpya wa mahakama hiyo.
Wagombea tisa ikiwa ni pamoja na majaji wawili mmoja kutoka Nigeria na mmoja kutoka Uganda, wako katika orodha ya kumrithi Mgambia, Fatou Bensouda, ambaye muhula wake kama Mwendesha mashitaka Mkuu wa Mahakama hiyo unamalizika mwezi Juni mwaka huu.
Bensouda amekuwa Mwendesha mashitaka Mkuu wa ICC tangu mwaka 2011 baada ya kuchukua nafasi ya wakili, Muargentina Luis Moreno Ocampo.
Katika muhula wake madarakani, aliweza kuwatia hatiani washitakiwa zaidi kuliko mtangulizi wake na hivi karibuni akiwa ni muasi wa zamani wa Uganda, Kamanda Dominic Ongwen, ambaye mwezi huu alipatikana na hatia za uhalifu wa kivita.
Hata hivyo alikabiliwa na ukosoaji mkubwa hususan ni kuhusu kesi zake kuwalenga Waafrika.
Juni mwaka jana, Bensouda alizuiwa kusafiri nchini Marekani wakati rais wa Marekani wa wakati huo, Donald Trump aliposaini sheria ya rais inayoweka vikwazo vya fedha dhidi yake.
Watu wengine wanaowania nafasi ya Bensouda ni pamoja na:
1:Karim Khan– Wakili Kutoka
2. Robert Petit, Mwendesha mashitaka kutoka Canada
3.Susan Okalany– Jaji kutoka Uganda
4. Morris Anyah- Jaji kutoka
5. Fergal Gaynor – mwendesha mashitaka kutoka IRELAND
6. Fernandez Castresana- mwendesha mashitaka kutoka Uhispania
7. Francesco Lo Voi- mwendesha mashitaka kutoka Italia.
8. Brigitte Raynaud – mwendesha mashitaka kutoka Ufaransa
9. Richard Roy – wakili kutoka Canada