25.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Iran yavunja mkataba wa nyuklia kwa kurutubisha Uranium

Tehran, Iran

Iran imeanza kutengeneza madini ya uranium, licha ya kuonywa na mataifa yenye nguvu duniani kwamba ni uvunjaji mwingine wa mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015.

Wakaguzi wa Shirika la kimataifa la udhibiti wa nguvu za atomi wamethibitisha uwepo wa gramu 3.6 (0.1oz) za madini hayo katika kiwanda cha Isfahan wiki iliyopita.

Iran inasema inafanya utafiti na kutengeneza madini hayo kwa lengo la kutengeneza mafuta kwa ajili ya utafiti wa mitambo.

Lakini chuma cha uranium kinaweza pia kutumika kutengenezea bomu la nyuklia.

Iran inasisistiza kuwa mpango wake wa nyuklia ni wa amani, lakini imekiuka makubaliano kadhaa katika mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 katika kipindi cha miaka miwli iliyopita.

Inasema inakiuka mkataba huo kujibu hatua ya Marekani kuiwekea vikwazo vya kiuchumi ambavyo vilirejeshwa tena mwaka 2018 na aliyekuwa rais wa Marekani wakati huo Donald Trump wakati alipovunja mkataba huo kwa kujiondoa.

Mrithi wake, Joe Biden, anasema Iran lazima irejee katika kuheshimu kikamilifu mkata wa nyuklia kabla ya kuondolewa vikwazo. Lakini kiongozi wa ngazi ya juu zaidi wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, anasema Marekani lazima iondoe vikwazo kwanza.

Chiia ya mkataba huo Iran ilikubali kutotengeneza uranium au kufanya utafiti na kutengeneza madini hayo kwa muda wa miaka 15.

Siku ya Jumatano jioni Shirika la Umoja wa Mataifa la udhibiti nishati ya nyuklia (IAEA) lilisema kuwa mkurugenzi wake mkuu aliwafahamisha wajumbe wa mataifa “kuhusu shughuli za hivi karibuni za Iran za kutengeneza chuma cha uranium kama sehemu ya kile ilichosema, yanatumiwa katika kutengeneza mafuta kwa ajili ya utafiti wa mitambo ya Iran “.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles