23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Taasisi ya Saratani Ocean Road yapokea mashine ya kisasa ya kutambua saratani

Na Faraja Masinde, Dar es Salaam

Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) ya jijini Dar es Salaam imepokea msaada wa mashine ya kisasa yenye uwezo wa kupima uvimbe na kutambua moja kwa moja kama ni saratani ndani ya muda mfupi.

Msaada huo umetolewa Februari 11, mwaka huu hospitalini hapo na Taasisi ya Mradi Mtambuka wa Saratani Tanzania (TCCP) na kwamba itasaidia kupunguza muda wa wagonjwa kusubiri muda wa uchunguzi wa saratani.

Akizungumza mara baada ya kupokea Mashine hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ocean Road, Dk. Julias Mwaiselege amesema mashine hiyo ya kisasa itarahisisha utoaji wa huduma ikiwamo kuongeza idadi ya wagonjwa wnaopimw akutoka 50 hadi 80 kwa siku.

“Tunashukuru kwamba leo tumepata msaada huu wa mashine ya kisasa ya Saratani ambayo tunaamini kuwa itaenda kuongeza ufanisi na uharaka wa huduma, kama tunavyofahamu kwamba serikali imeboresha huduma za saratani ikiwamo mashine mbili za kisasa za tiba ya mionzi ambazo.

“Utoaji wa dawa pia umeongezeka kufikia asilimia 98 ambapo karibu Sh milioni 10 kimekuwa kikitengwa kwa ajili ya dawa za saratani,” amesema Dk. Mwaiselege.

Upande wake Meneja wa Mradi huo, Dk. Harrison Chuwa ambaye ni Meneja wa mradi huo amesema lengo la Matoaji wa mashine hiyo iliyogharimu Sh milioni 115 ni kuona uchunguzi wa huduma za saratani ukifanyika kwa haraka.

“Lengo ni kuendelea kuboresha miundombinu ya utoaji wa matibabu ya saratani hapa nchini na hili tumelidhihirisha leo kwa kuiletea taasisi kongwe ya Ocean Road mashine hii ya kisasa ambayo inatumia teknolojia ya juu na ya kisasa zaidi ambayo mi ya njia ya mawimbi na sauti,” amesema Dk. Chuwa.

Upande wake Meneja wa kitengo cha Mionzi wa Hospitali ya Ocean Roada, Dk. Revelian Iramu amesema mashine hiyo ina uwezo wa kuonyesha uvimbe kwa teknolojia ya juu na hivyo ukapata saizi kalimili ya ule uvimbe ikilinganishwa na mashine zilizokuwepo awali.

Aidha, mradi Mtambuka wa Saratani Tanzania (TCCP) umezindua nembo ya mradi na kukabidhi mashine ya Radiolojia kwa njia ya mawimbi sauti (3D Ultrasound) kwa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI).

Mradi huo unaendeshwa na Huduma za Afya za Aga Khan, Tanzania, na washirika kiutendaji ambao ni, Hospitali ya taifa Muhimbili, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road na Hospitali ya Rufaa ya Bugando, ukiwa umejidhatiti katika kusaidia juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya saratani Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Hii mashine imetengenezwa na wataalamu wetu hapa nchini au? Kama imetoka kwa wazungu tunawezaje kuamini kuwa haina kasoro? Kwanini tusitumie dawa zetu za kijadi badala ya kuwategemea wazungu?

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles