27.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yang’ara tuzo ya vivutio bora vya utalii dunini

Na Victor Makinda, Morogoro

 Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, imepigiwa kura na kushinda kuwa mbuga bora zaidi ya hifadhi ya wanyama duniani.

Hayo yamesema  mapema leo Machi 3, 2021 mjini Morogoro na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbalo wakati wa maadhimisho ya siku ya wanayamapori duniani yaliyokwenda sambamba na mkutano wa wadau wa sekta ya utalii.

Akizungumza katika hafla hiyo Dk. Ndumbalo alisema Tanzania imeshinda tuzo hiyo na kuwa ya kwanza kupitia hifadhi ya Taifa ya Serengeti, huku Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Mlima Kilimanjaro zikiwa zimeshika nafasi za juu katika tuzo hizo ambazo hutolewa na Chief Traveler Award (CTA).

“Yalichaguliwa maeneo 25 yanayovutia zaidi kwa utalii kote duniani, katika hayo maeneo matatu yametoka Tanzania, ambapo eneo la kwanza lililopigiwa kura na kushinda kwa kuwa kivutio bora zaidi duniani ni, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, huku hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na Tarangire zikiwa ni miongozi mwa maeneo bora zaidi ya utalii,” alisema Dk. Ndumbalo.

Dk. Ndumbalo amesema kuwa mafaniko hayo hayakuja tu bali yametoka na mikakati ya dhati ya serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi shupavu wa Rais Dk. John Magufuli katika uwekezaji na usimamizi madhubuti ya hifadhi za zetu za Taifa.

Dk. Ndumbalo ametoa wito kwa Watanzania, kujivunia mafanikio hayo huku wakifanya kila linalowezekana kuvitangaza vivutio hivyo vya utalii mahali pote duniani kwa lengo la kuzidi kukuza utalii na kuueleza ukweli Ulimwengu juu ya ubora wa vivutio vilivyopo nchini kwetu.

Katika hatua nyingine Dk. Ndumbalo, aliwaonya watu wote wanaofanya shughuli za kibiniadamu maeneo ya hifadhi, ikiwa ni kilimo au ufugaji, kuacha mara moja kwa serikali itakapowabaini itawachukulia hatua kali za kisheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles