30.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

BoT: VICOBA visivyosajiliwa mwisho Aprili 30

Na Sheila Katikula,Mwanza

Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mabenki  kutoka Benki Kuu, Jerry Masyenene, amesema  ifikapo Aprili 30, mwaka huu vikoba ambavyo havijasajiliwa havitatambulika katika sekta ya fedha.

Masyenene amebainisha hayo katika ufunguzi wa mafunzo ya miongozo na mfumo wa usajili wa vikundi  vya kijamii vya huduma ndogo za fedha uliofanyika mkoani Mwanza.

Akizungumza na Maafisa Tehama na  Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka Mikoa ya Mwanza, Kigoma na Shinyanga amesema agizo hilo linazingatia sheria mpya ya huduma za fedha ya mwaka 2018 benki kuu ndiyo maana imetoa mafunzo hayo kwa maafisa hao.

Amesema faida za kusajili vikoba ni pamoja na kupunguza wimbi la umasikini katika jamii,kutengeneza mamilionea  na kupata mikopo kwa haraka kutokana na kutambulika katika sekta za kifedha.

Amesema kila kikundi kinapaswa kuwa na wanachama wasiopungua 10 na wasiozidi 50 tofauti na hapo hakitasajiliwa, hakuna gharama ya usajili na kila kikundi kitatakiwa kuwa na katiba ambayo imepitishwa kwenye mkutano Mkuu mmoja na kutakuwa na mkaguzi wa kikundi  na ukaguzi kutoka Tamisemi.

“Na baada ya usajili watapewa cheti kutoka kwa Mkurugenzi  wa Halmashauri kupitia vikundi hivyo tutapata mabilione kwani huko nyuma walikuwa wakitapeliwa fedha zao kwa sababu ya kukosa mfumo wa kielektroniki  kupitia  sheria  hiyo ya usajili wa vikundi utawaweka salama ili kuendelea kunufaika  kwenye vikundi vyao.

Amesema huko nyuma kulikuwa na makampuni mengi yanayotoa mikopo lakini hakukuwa na usimamizi wowote  kwani hivi sasa kampuni zote zinazotoa mikopo  zipo chini ya usimamizi wa banki kuu kwani imetengeneze nyaraka  zote muhimu zitakazosimia vikundi hivyo. 

Naye Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanel Kipole, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela amewata Maafisa Maendeleo ya Jamii Maafisa Tehama kuwashirikisha elimu waliyoipata  watendaji wa kata, mtaa navijiji  kwa  sababu vikundi hivyo huanzia huko no vema kuhakikisha zoezi hilo linasimamiwa ili kupunguza kiwango cha umasikini kwenye  Maene yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles