23.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

Katibu Mkuu mpya Biashara United kuendelea malengo

Na Shomari Binda, Mara

Katibu Mkuu mpya wa Klabu ya Biashara United, Haji Mtete, ameahidi kufikia malengo ya timu hiyo kumaliza ligi katika nafasi tano za juu kama walivyojiwekea.

Akizungumza na www.mtanznaia.co.tz baada ya kuthibitishwa na Kamati Tendaji ya timu hiyo kushika nafasi hiyo amesema lengo la klabu bado liko palepale.

Amesema licha ya ligi kuwa ngumu katika kipindi hiki cha mzunguko wa pili lakini watapambana kuhakikisha lengo linafikiwa.

Mtete amesema atahakikisha anashilikuana vyema na viongozi,wanachama pamoja na wadau m alimbaoi ili kuifanya Biashara United kuwa moja ya timu kubwa hapa nchini.

Amesema katika masuala ya uongozi hasa wa michezo anao uwezo na uzoefu ambao utamsaidia kutimiza wajibu wake.

“Numeaminiwa kupewa nafasi hii nami naahidi kuitendea haki kwa kuhakikisha malengo ya klabu ikiwemo kumaliza katika nafasi za juu kwenye ligi yanafanikiwa.

“Kikubwa naomba ushirikiano kutoka kwa viongozi wenzangu,wanachama pamoja na wadau ili malengo yetu yaweze kufanikiwa,” amesema Mtete.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Timu hiyo, Selemani Mataso, alisema watampa Katibu huyo ushirikiano wa kutosha katika kutimiza wajibu wake.

Timu ya Biashara United inayoshika nafadi ya nne kwenye msimamo wa ligi imeelekea mkoani Morogoro ambapo Machi 4, itashuka katika dimba la Jamhuri kucheza na Mtibwa Suger.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles