Na Brighiter Masaki
Mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Quraan tukufu 2019 yatakayoshirikisha nchi zaidi ya 30 zikiwemo Tanzania, Saud Arabi, Marekani, Australia, Canada, Uingereza, India na Urusi, yatafanyika Tanzania Mei 21 hadi 26.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa mashindano hayo, Jumuiya ya kuhifadhi Quraan Tanzania Sheikh Othman Ally, amesema kuwa mashindano hayo yataanzia katika nchi husika na baadae kuhitimishwa katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar Es Salaam.
“Mashindano haya kwa mwaka huu yatafanyika hapa nchini kimataifa na kushirikisha nchi 30 ikiwemo Tanzania yenyewe. Mashindano yataanza kwenye nchi husika na kwetu yataanzia mikoani na baadae kilele cha tuzo hizi kitafanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo atapatikana mshindi wa jumla wa tuzo, mashindano haya ni kwa watoto kuanzia mwaka mmoja hadi kumi” alisisitiza Sheikh Ally
Aliongeza kuwa mashindano hayo yamegawanyika katika vipengele vitatu, kitaifa yani Tanzania peke yake, Afrika Mashariki na dunia ambapo zinahusisha nchi zisizopungua 30.