27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Quraan 2019

Na Brighiter Masaki

Mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Quraan tukufu 2019 yatakayoshirikisha nchi zaidi ya 30  zikiwemo Tanzania, Saud Arabi, Marekani, Australia, Canada, Uingereza, India na Urusi, yatafanyika Tanzania Mei 21 hadi 26.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa mashindano hayo, Jumuiya ya kuhifadhi Quraan Tanzania Sheikh Othman Ally, amesema kuwa mashindano hayo yataanzia katika nchi husika na baadae kuhitimishwa katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar Es Salaam.

“Mashindano haya kwa mwaka huu yatafanyika hapa nchini kimataifa na kushirikisha nchi 30 ikiwemo Tanzania yenyewe. Mashindano yataanza kwenye nchi husika na kwetu yataanzia mikoani na baadae kilele cha tuzo hizi kitafanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo atapatikana mshindi wa jumla wa tuzo, mashindano haya ni kwa watoto kuanzia mwaka mmoja hadi kumi” alisisitiza Sheikh Ally

Aliongeza kuwa mashindano hayo yamegawanyika katika vipengele vitatu, kitaifa yani Tanzania peke yake, Afrika Mashariki na dunia ambapo zinahusisha nchi zisizopungua 30.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles