27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania kusaka tiketi ya kufuzu Paralimpiki

Na Victoria Godfrey, Dar es Salaam

Tanzania inatarajia kushiriki Mashindano ya Dunia kwa ajili ya kufuzu kwa michezo ya Paralimpiki itakayofanyika Nchi tofauti tofauti.

Michezo ya Paralimpiki imepangwa kuanza kutimua vumbi Agosti 24 hadi Septemba 5, mwaka huu mji wa Tokyo, Japan.

Katibu Mkuu wa Kamati ya Paralimpiki Tanzania (TPC), Ramadhan Namkoveka, amesema michezo ambayo kamati imeipa kipaumbele ni riadha, mchezo wa kunyanyua vitu vizito na kuogelea kwa watu wenye Ulemavu.

“Tanzania tunatarajia kupeleka wachezaji nane wa michezo mitatu, hivyo maandalizi yanaendelea kufanyika na wachezaji wanafanya mazoezi ya kutosha ili kuweza kufikia malengo yetu ya kufuzu,” amesema Namkoveka.

Amesema mashindano hayo yanafahamika kama Tunis 2021 World Para Athletics Grand Prix – TUNISIA – yatakayofanyika kuanzia Machi 14 hadi 21 mwaka huu nchini humo

“Michezo mingine ni kunyanyua vitu vizito ambayo imepangwa kufanyika Juni 16 hadi 21, Mwaka huu katika nchi za olombia, Thailand, Uingereza, Gerogia na Falme za Kiarabu katika Jiji la Dubai.

Ameongeza kuwa mengine ni kuogelea yamepangwa kufanyika Aprili 8 hadi 11, mwaka huu, Sheffield, Uingereza, na mengine yatafanyika Aprili 15 hadi 17 mwaka huu, Lewisville, na Dallas Taxes nchini Marekani.

Amefafanua kuwa kabla ya michezo ya Paralimpiki wachezaji wanatakiwa kushiriki ‘classification’ ili kuainisha aina yake ya ulemavu na atashiriki kundi gani la watu wenye ulemavu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles