26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yatoa wito kwa waandaji wa Kili Marathoni

Na Safina Sarwatt, Kilimanjaro

Serikali imetoa wito kwa waandaji na Chama cha Riadha kuwaanda washindi wa mbio za Kilimanjaro Marathon ili waweze kushiriki mashindano ya Kimataifa ya Olimpik.

Akizungumza katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi hafla kutoa zawadi kwa washindi mbio za Kilimanjaro Marathon Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Abdallah Ulega, amesema Serikali inataka kuona idadi ya washiriki mbio za Kimaifa za Olimpik inaongezeka.

Ulega amesema makampuni yaliyoandaa mashindano ya mbio za Kilimanjaro ikiwemo kampuni ya bia ya Kilimanjaro, Tigo kuwadhamini wanariadhaa hao waweze kushiriki mbio za Olimpiki.

“Washindi hao watakuwa katika kambi ya timu ya taifa ili waweze kufanya mazoezi zaidi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano kimataifa.

“Leo nimeshuhudia vipaji kweli kweli na wale walioneka kufanya vizuri katika mashindano hayo serikali imeelekeza waongezwe kwenye timu ya taifa ya Olimpiki, Watanzania wameng’ara  katika mbio za Kilimanjaro marathon kilometa 42 na 21 upande wanaume na wanawake baada kuongoza nafasi za kwanza hadi kumi bora,” amesema Ulega.

Katika mbio za kilometa 42 upande wa wanaume mshindi wa kwanza ni Mtanzania, Augustino Sulle, ambaye ametumia masaa 02:18:04 mshindi wa pili, Michael Sanga, aliyetumia masaa 02:19:21, mshindi wa tatu ni Charles Sulle aliyetumia masaa 02:20:21.

Upande wanawake mshindi wa kwanza ni Jackline Sakilu, ametumia masaa 02:45:44, mshindi wa pili Catherine Yuku, ametumia masaa 02:59:06, na mshindi watatu Mary Xwaymay ametumia masaa 03:07:28.

Katika mbio za kilometa 21 wanaume mshindi wa kwanza, Abel Chebet, kutoka Uganda ametumia saa 01:03:17, Gabriel Geay Mtanzania ametumia saa 01:03:18, mshindi wa tatu, Emmanuel Giniki, mtanzania ametumia saa 01:03:31.

Upande wanawake kilometa 21 mshindi wa kwanza Failuna Matanga mtanzania ametumia saa 01:16:17 ,mshindi Angelina Tsere mtanzania ametumia saa 01:17:43,mshindi wa tatu Anstasia Dolomongo mtanzania ametumia saa 01:18:13.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles