23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Huawei yaunga mkono malengo ya Maendeleo Endelevu ya UN

Shanghai, China

Kampuni ya Huawei imeunga mkono Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (UN SDGs) katika kujenga ulimwengu wa kijani, ubunifu na umoja ikiwa kampuni hiyo ya teknolojia pia inaamini teknolojia inaweza kufanya kazi kama injini ya maendeleo ya binadamu.

 Akizungumza katika Mkutano wa masuala ya Ushirikiano, ukuaji na Ufanisi katika masuala ya teknolojia uliofanyika Shanghai, Makamu wa Rais mwandamizi wa Huawei na mjumbe wa bodi Catherine Chen, alisema teknolojia inaweza kuwa injini ya maendeleo ya binadamu, na akatoa wito kwa watu binafsi na wafanyabiashara kufikiria mambo kwa ukubwa zaidi na kutenda kidogo.

Makamu wa Rais Mwandamizi wa Kampuni ya Huawei ambaye pia ni Mjumbe wa bodi ya Huawei, Catherine Chen.

Chen alisema ni muhimu kwamba watu wawe  karibu zaidi na teknolojia, ambayo kimsingi inaweza kuwa nguzo sahihi ya kufanika kufikia malengo ya maendeleo.

 “Mabadiliko makubwa ya kijamii huwa yanatokea kwa njia ya kuambukizana na mafanikio katika sayansi na teknolojia. Lakini leo, maendeleo ya kiteknolojia yanayoripotiwa ni ya kisiasa – kama wakati mwingine imekuwa hivyo kwa teknolojia 5G,” amesema.

Chen amesema teknolojia ya 5G ilikuwa teknolojia sanifu iliyofafanuliwa na upeo wake wa juu na muunganisho mpana, ambao unaweza kubadilisha tasnia za jadi na kufaidisha wote.

 “Kila siku, watumiaji wananufaika na ufanisi wa teknolojia ya 5G, wakati matumizi ya viwandani kwenye bandari, migodi, na sekta ya uchukuzi inaongeza ufanisi wa utendaji. Je! Hili ni jambo baya? Sidhani hivyo,” amesema.

Chen alisema kuwa wakati kila wakati kumekuwa na tishio kwamba teknolojia mpya inaweza kutumiwa vibaya, sheria zinaweza kuanzishwa kudhibiti hatari za kiteknolojia.

“Watu wengi tayari wana bidii kazini kuunda sheria za utawala kwa usalama wa mtandao, ulinzi wa faragha, na yote ambayo yatatuweka salama. Kwa sisi wengine, ni wakati wa kujiamini na kufungua maendeleo ya teknolojia,” ameongeza.

 Chen alielezea jinsi Huawei ilivyo tayari kupeleka suluhisho za kidijiti kuwawezesha watu na kufikia malengo ya maendeleo ya UN – haswa malengo ya uvumbuzi, usawa na elimu bora.

Kwa Afrika Kusini, kwa mfano, Huawei, shirika lisilo la faida la Click Foundation waliungana na kuunganisha zaidi ya shule 100 za msingi za mijini na vijijini kwenye huduma za internet. Lengo ni kuongeza ujuzi wa kusoma na kuziba pengo la dijiti kupitia teknolojia.

Nchini Kenya, Huawei ilishiriki katika kujenga Digitrucks, vyumba vya madarasa vinavyotumia umeme wa jua ambavyo huleta ustadi wa kidijiti kwa jamii za pembezoni, ambazo hazina huduma hiyo.

Chen pia alielezea namna Huawei Smart PV ivyotumiwa katika nchi zaidi ya 60 ikiwa tayari imesaidia kufikia SDGs, na imepunguza uzalishaji wa kaboni kwa kiasi cha tani milioni 148.

 â€œHii ni sawa na kupanda miti zaidi ya milioni 200. Nchini Ethiopia pekee, tumesaidia wateja wetu kupeleka zaidi ya vituo 400 vya umeme wa jua, kupunguza uzalishaji wa kaboni kwa tani 2 850. Nchini China, tumesaidia pia kujenga vituo vikubwa zaidi vya jua maalum kwa kilimo na uvuvi katika miji wa Ningxia na Shandong. “

Huawei na UNESCO pia wameshirikiana kuzindua mpango wa Shule uria kwa kuwezesha  shule za Misri, Ethiopia, na Ghana kuboresha ujuzi wao wa kidijiti kupitia elimu ya mtandaoni.

 “Katika mifano hii yote kila unganisho, kila gramu ya uzalishaji imepunguzwa, kila wati ya umeme iliyookolewa, haingeweza kupatikana bila maendeleo madogo katika teknolojia,” alisema Chen.

 “Hii ndio thamani ambayo teknolojia inaleta ulimwenguni,” amehitimisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles