29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Prof. Kitila aongoza ziara ukaguzi miradi mfuko wa jimbo

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Mfuko wa Kuchochea Maendeleo Jimbo la Ubungo, Profesa Kitila Mkumbo, amewaongoza wajumbe wa mfuko huo kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ambayo inatarajiwa kupatiwa fedha na mfuko huo.

Katika ziara hiyo Profesa Kitila aliambatana na wajumbe wa Mfuko huo wa Jimbo ambao ni Diwani wa Kata ya Makurumla, Bakari Kimwanga, Diwani wa Viti Maalumu, Hawa Abdulrahman.

Mwenyekiti wa Mfuko wa Kuchochea Maendeleo Jimbo la Ubungo ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Profesa Kitila Mkumbo, akisisitiza jambo wakati wa ukaguzi huo Februari 27, 2021.

Wengine ni Isihaka Waziri, Rozina Kimario pamoja na mchumi, ambapo hatua hiyo imetokana na uamuzi wa kamati hiyo kutembelea miradi yote kwenye jimbo kabla ya kuanza kutoa fedha.

Kutokana na changamoto kadhaa zilizopo katika kata nane za Jimbo la Ubungo ambazo ni Ubungo, Kimara, Makuburi, Sinza, Mburahati, Makurumla, Mabibo na Manzese wajumbe kwa kauli moja waliamua kwenda kufanya ukaguzi wa miradi hiyo ili kujiridhisha kama ina vigezo vya kusaidiwa kwa haraka.

Katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Mfuko wa Kuchochea Maendeleo Jimbo la Ubungo, Profesa Kitila aliwaambia wananchi wa kata za Makurumla, Manzese na Mabibo kuwa Serikali imetoa kiasi cha Sh milioni 70.6 kwa ajili ya kuchochea maendeleo kwenye jimbo hilo.

Mjumbe wa Mfuko huo wa Jimbo ambae ni Diwani wa Kata ya Makurumla, Bakari Kimwanga, akionyesha jambo wakati wa ziara hiyo.

Amesema wajumbe kwa kauli moja wamekubaliana kutoa kipaumbele cha fedha katika miradi ya elimu, afya na miundombinu hasa ya babarabara na vivuko ambavyo vimekuwa kero kubwa kwa wananchi.

“Tumetembea hapa Mto China na tumeona hali ya takataka zinazosafirishwa na maji namna zilizoziba mto nasi kupitia Mfuko wa Jimbo tutaingiza kiasi cha fedha ili kisaidie kazi hii ambayo chini ya diwani ataisimamia. Pia tutasaidia barabara muhimu ya kwa Mloka Mtaa wa Kilimahewa ila kubwa tunawaomba watalaamu wa Tarura watusaidie gharama ili tuweze kukamilisha kazi hii kwa wakati.

“Tunataka fedha hizi zinazotolewa na Serikali ziende zikaguse maendeleo ya wananchi moja kwa moja,nasi kupitia Kamati ya Mfuko wa Jimbo kila senti ambayo tutapokea kutoka serikalini tutaweka wazi na wala si kificho,” amesema Profesa Kitila

Pamoja na hali hiyo wajumbe hao walitembelea Kata ya Mabibo na kuona athari za Mto Gide pamoja na Mto Mbokomu Kata ya Manzese

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles