25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania ‘Amateur Stroke Play’ yaanza rasmi Kilimanjaro

Na Mwandishi Wetu

ZAIDI ya wachezaji 20 wa gofu  wameanza kuchuana katika mashindano  yajulikanayo kama Tanzania  ‘Amateur Stroke Play’ liloanza leo Novemba 26,2021 kwenye  viwanja vya TPC mkoani Kilimanjaro.

Katika michezo ya ufunguzi kwa wachezaji wa kulipwa, Frank Mwinuka wa Lugalo ameongoza kwa mikwaju 72 akifuatiwa na Nuru Mollel wa Arusha Gymkhana aliyepiga mikwaju 73, huku Bryson Nyenza wa Lugalo akimfunga Hassan Kadio wa Dar Gymkhana kwa mikwaju 74.

Wakizungumzia michuano hiyo itakayofanyika kwa siku tatu mfululizo, baadhi ya wachezaji kutoka vilabu mbalimbali wamesema ushindani ni mkubwa ukilinganisha na mashindano mengine.

Akizungumzia mchezo wake, Rajab Pembe kutoka Dar Gymkhana amesema ameanza vibaya anasubiri kesho kuona kama atafanya vizuri.

“Waandaji wamefanya maandalizi mazuri ya uwanja ni mzuri, shimo ziko vizuri, mtu akicheza vibaya ajilaumu mwenyewe,” amesema Ally Mwinyi kutoka TPC Klabu.

Michuano  itaendelea kesho kwa wachezaji wa kundi B na C ambapo litahitimika jumapili Novemba 28,2021 likihusisha klabu ya Lugalo, Dar Gymkhana, Moshi Klabu, Kili Gofu, Arusha Gymkhana, Morogoro, Mufindi na wenyeji TPC.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles