21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

TANGO HUSAIDIA KUONDOA SUMU MWILINI

Na HERIETH FAUSTINE


 

tangoTANGO ni tunda ambalo hupatikana katika maeneo mengi duniani lakini limekuwa halitiliwi mkazo katika kulila.

Matango yana uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali kwa njia rahisi isiyokuwa na madhara kwa mtumiaji, kutokana na matibabu yake kuwa rahisi na hupatikana kwa bei nafuu.

Wataalamu mbalimbali wanasema kuwa tango lina faida kubwa katika mwili wa binadmu kutokana na kuwa na aina mbalimbali za vitamin B, B Complex, C na E pamoja na madini ya Potassium, Zinki, Chuma, Kambalishe na Kashium.

Tango husaidia kuboresha kiwango cha maji ambayo huitajika mwilini, hii ni kutokana na matango kuwa na kiwango kikubwa cha maji ambacho ni asilimia 95, maji haya husaidia kuondoa taka mwili pamoja na sumu mbalimbali ambazo huingia mwilini kupitia katika vyakula, vinywaji na madawa.

Pia tango husaidia kupunguza uzito wa mwili kutokana na kuwa na asili ya nyuzinyuzi ambazo humfanya mlaji ajisikie kushiba bila ya kuongeza vitu mwilini.

Vilevile husaidia kuondoa sumu mwilini na kurahisisha ufyonzwaji wa protini kutokana na uwepo wa kiwezeshaji kinachoitwa erespin enzyme.

Tunda la tango pia husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani, kwa kuweka kipande cha tango mdomoni kwa dakika tano mara tatu kwa siku husaidia kuua bakteria mbalimbali wasababishao magonjwa mbalimbali ya kinywa.

Kutokana na tango kuwa na vitamin B, husaidia kupunguza uchovu, mawengewenge pamoja na hali ya kujisikia vibaya kutokana na unywaji wa kilevi.

Vilevile ulaji wa matango na husaidia kuondoa msongo wa mawazo na kuboresha utendaji wa   mishipa mbalimbali ya fahamu mwilini na hivyo kuondoa hatari ya mtu kuathirika na msongo wa mawazo unaosababishwa na maisha ya kila siku.

Husaidia kuondoa hatari ya mtu kupata kansa kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha virutubisho vyenye asili ya mimea pamoja na vitamini C ambayo husaidia kuondoa sumu mbalimbali na kuboresha kinga ya mwili.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles