28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Tanesco yawanasa wachepusha umeme Dar

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeanza operesheni na kuwanasa wachepusha umeme kadhaa eneo la Kinondoni Kaskazini.

Operesheni hiyo imeanza jana ambako wateja kadhaa wamebainika kufanya vitendo hivyo vya kuchepusha umeme   usipite kwenye mita kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa matumizi yake na hivyo kuliibia shirika hilo.

Kaimu Meneja wa TANESCO anayeshughulikia Wateja Wakubwa,   Frederick Njavike, alikuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari baada ya ukaguzi huo wa kushtukiza.

Alisema si tu wateja binafsi wanaofanya hujuma hizo  lakini pia taasisi za umma likiwamo shirika moja la umma (jina linahifadhiwa).

 Njavike alisema kwa kawaida kila mwisho wa mwaka shirika hupanga siku za kufanya ukaguzi wakushtukiza  kuangalia sehemu gani TANESCOinapoteza mapato.

 “Tumekuta kuna miundombinu ya TANESCO imechezewa na mbaya zaidi ni kwamba hata taasisi za umma zinashiriki vitendo hivyo.

“Wito wetu tunaomba taasisi zote za serikali kujaribu kupitia miundombinu yote ya umeme na vilevile kuangalia watu waliowapangishakwenye vitega uchumi vyao,” alisema.  

Alisema TANESCO ni shirika la umma hivyo amewaomba wateja na wasio wateja kutoa taarifa kwa wale wote wanaochezea miundombinu kwa  vile watakuwa wamesaidia shirika lao kuokoa fedha kutokana na wizi huo.

Ofisa wa Usalama wa shirika hilo, Mkoa wa Kinondoni,Mohammed Mtoro alisema zipo hatua mbalimbali ambazo TANESCO huchukua dhidi ya vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na kusimamisha huduma pamoja wahusika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles