Na Asha BÃ ni -Dar es salaam
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Wilaya ya Ilala inatoa rai kwa wananchi wanaohujumu shirika hilo kwa kujiunganishia umeme kwa kutumia vishoka ili kukwepa ulipaji kwenye mita kuacha mara moja.
Tanesco ilala imefanya ziara ya kushtukiza katika Ofisi ya kampuni ya Wakala wa usafirishaji abiria kwa ndege ( Cosmos Travel Agency) na kubaini kujiunganishia umeme kwa njia ya wizi iliyofanywa na kampuni hiyo.
Msimamizi wa Kitengo cha kudhibiti Mapato wa shirika hilo Wilaya ya Ilala,Bernad Mshilimu akiwa eneo la Mbuyuni Posta alifanya ziara na ukaguzi wa kushtukiza na kubaini mteja kajiunganishia umeme moja kwa moja kutoka Tanesco bila kupita kwenye mita ya Luku kinyume na utaratibu.
Aliongeza kuwa kitendo hiko kinawanyima mapato shirika yake na kudhorotesha Huduma katika baadhi ya maeneo.
Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja Ilala Deusdedit Hokororo alisema hiyo ni kawaida kwa shirika kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha wahujumu wa shirika wanakamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki.
Hokororo aliwataka mmwananchiwengine wanapopata taarifa za wizi wa umeme au hujuma kutoa tariarifa kwao ili waweze kulishughulikia na kuwabaini.
“Wananchi wema watakaotoa tarifa hizo watalindwa na itakua siri kati yao na Tanesco ,lengo watu wasilihujumu shirika kwa kuwa linategemewa nchi nzima na umuhimu mkubwa,”alisema Hokororo.