30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Tandale waitupia lawama Manispaa ya Ubungo kushindwa kufanya usafi

NEEMA SIGALIYE na FAUSTINE MADILISHA (TUDARCO) –dar es salaam

WAFANYABIASHARA wa soko la Tandale wameilalamikia Manispaa ya Ubungo kwa kushindwa kufanya usafi katika soko hilo, hali inayosababisha kuwa kero kwa wafanyabiashara na wateja  sokoni hapo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu msaidizi wa soko hilo, Marco Kidakule, alisema wamekuwa wakichanga fedha kwa usafi, lakini haufanyiki.

Alisema uchafu katika soko hilo, unatokana na kutokuwapo kizimba cha kuwekea takataka pamoja na manispaa kushindwa kutimiza wajibu wake.

“Licha ya fedha za takataka kutolewa, tumekuwa na changamoto ya magari kutofika kwa wakati,” alisema Kidakule.

Alisema uongozi wa soko uliweka utaratibu wa kufanya usafi, lakini tangu manispaa ichukue mamlaka ya kusimamia usafi hali imekuwa mbaya.

“Tulikuwa na kamati ya usafi ya soko ambayo ilikuwa inakusanya fedha za usafi na kuweka watu ili wafanye usafi sokoni, manispaa sasa ndiyo msimamizi, imeshindwa kutimiza wajibu wake,” alisema.

Meneja wa soko hilo, Ahmed Ramadhani, alisema fedha za usafi hukusanywa, lakini hakuna kinachofanyika.

“Sokoni huwezi kufanya usafi asubuhi kwa sababu ndio muda magari yanaingiza mizigo, tunafanya usafi saa 8 mchana kila siku japo tunachangamoto ya uhaba wa magari ya kubebea takataka,” alisema Ramadhani

Alisema kuwalaumu wananchi wa eneo hilo, ndiyo chanzo kikubwa cha uzalishaji takataka katika soko hilo kwa kuwatumia mateja nyakati za usiku kutupa maeno ya sokoni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles