24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

Raia wa Malawi apandishwa kizimbani

ERICK MUGISHA na BOSCO MWINUKA (TUDARCo)-DAR ES SALAAM

RAIA wa Malawi, Paul John (30), amepandishwa kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam kwa kosa la kujiridhisha kingono.

Akisomewa hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Esther Mwakalinga, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Hellen, alidai Machi 25, mwaka huu eneo la Tegeta Nyuki wilayani Kinondoni, Dar es Salaam mshtakiwa alimuingiza vidole sehemu za siri mtoto wa miaka 7.

Mshtakiwa alikana kutenda shtaka na Hakimu Mwakalinga alisema dhamana ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili Watanzania,  wafanyakazi wa taasisi inayotambulika kisheria, barua kutoka kwa waajiri wao na vitambulisho vya kazi.

Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi kesi yake itakapokuja kusomwa tena Septemba 10.

Wakati huo huo, mkazi wa Boko cha Simba, Ramadhan Jabiri (24), maarufu Pengo, amepandishwa kizimbani katika mahakama hiyo kwa kosa la mauaji.

Akisomewa hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Esther Mwakalinga, Mwendesha Mashtaka wa Serikali Hellen alidai Julai 30, mwaka huu  eneo la Boko cha Simba wilayani Kinondoni, Dar es Salaam mshtakiwa alimuua Haban Khalid.

Hellen alidai upelelezi wa shauri hilo unaendelea na anaomba tarehe nyingine kwa kusikilizwa tena kesi.

Hakimu Mwakalinga alisema mshtakiwa hataruhusiwa kujibu chochote kwa muujibu wa sheria hadi kesi yake itakapohamia Mahakama Kuu.

“Kesi hii haina dhamana, mshtakiwa atakuwa akitokea rumande hadi mwisho wa kesi na itakuja kusikilizwa tena Septemba 10, mwaka huu,” alisema Hakimu Mwakalinga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles