28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

TAMWA: Tunalaani vikali vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto

Mkurugenzi Mtendaji-TAMWA, Edda Sanga
Mkurugenzi Mtendaji-TAMWA, Edda Sanga

Chama cha Wanahabari Wanawake nchini (TAMWA) kinalaani vikali vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto ambao umekuwa ukifanyika nchini hasa ubakaji na ulawiti wa makusudi ambao wakati mwingine watu hubakwa na kuawa.

Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Eda Sanga, Edda Sanga, amesema kuwa matukio ya ubakaji, ulawiti na mauaji kwa wanawake na watoto yamekuwa yakifanyika kwa kasi ambapo hivi karibuni lilitokea kwa msanii wa ngoma za asili na Bongofleva ambaye alikutwa amefariki dunia katika majaluba ya mpunga mita chache kutoka barabara ya Moshi-Arusha

Anaeleza kuwa kuwa kwa mujibu wa taarifa za upelelezi wa awali wa kipolisi zimeonyesha kuwa yalitokana na kupigwa, kubakwa na kunyongwa kisha kutupwa eneo la Makumira, Kata ya Usa River wilayani Arumeru, tukio ambalo TAMWA imelilaani vikali na kuomba jeshi la polisi kufuatilia kwa karibu ili kuhakikisha waliohusika wanatiwa mbaroni na kuchukuliwaa hatua kali za kisheria.

“Pia gazeti la Mtanzania la tarehe 26 Oktoba, mwaka huu lilimkariri Kamanda wa Polisi, mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa kuwa katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu, katika Manispaa ya Moshi pekee, matukio ya ubakaji yaliyoripotiwa ni zaidi ya 102 ambapo kati ya hayo 33 yalikuwa ni ya ulawiti,” alisema Sanga

Aidha tukio hilo la kinyama kwa msichana huyo ni miongoni mwa matukio mengi ya kikatili kwa wanawake na watoto hali ambayo inahatarisha na kutishia ustawi wa mwanamke huku baadhi ya vyombo vya habari vikiripoti kuwa vitendo vya ubakaji na ulawaiti  vimeongezeka kwa kasi.

“TAMWA inaamini kuwa sheria itafuata mkondo wake ili liwe fundisho kwa wanaoendelea kufanya ukatili wa kinyama kwa wanawake na watoto,” alisisitiza Sanga

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles