23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Balozi Mahiga ataja matishio ya dunia

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga

Na LEONARD MANG’OHA – DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga, amesema mabadiliko ya tabianchi ni miongoni mwa matishio matano makuu ya dunia.

Akizungumza Dar es Salaam juzi alipokuwa akihitimisha kongamano la kujadili tatizo la mabadiliko ya tabianchi lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), aliyataja matishio mengine kuwa ni umasikini, uvunjifu wa amani na ugaidi, biashara haramu ya dawa za kulevya na biashara ya binadamu.

“Kongamano hili lilikuwa linazungumzia maisha na masilahi ya wafugaji, wakiuliza makundi yaliyoachwa katika maendeleo mtasema wanawake, watoto, walemavu na wazee lakini wanaofuata hapo ni wafugaji.

“Hili janga la mabadiliko ya tabianchi si tu linaathiri Tanzania bali kila nchi hapa duniani kama ilivyo umasikini, tishio la amani na ugaidi na hii inatokana na kutokuelewa kwanini haya yanatokea,” alisema Balozi Mahiga.

Pia alisema nchi za Afrika zimekuwa waathirika wakuu wa mabadiliko ya tabianchi licha ya kuwa bara hilo si chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira ikilinganishwa na nchi zilizoendelea.

Alisema mwanzo kulikuwa na ubishani mkubwa baada ya na Ulaya kukataa kuwajibika kusaidia kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi.

“Lakini Desemba katika mkutano wa Paris, tulikubaliana nchi zilizoendelea katika viwanda zisaidie kupambana na tatizo hili, wanasaidia vipi? Tunahitaji wataalamu watakaotupatia ujuzi na teknolojia itakayotuwezesha kukabiliana na tatizo hili na kutuwezesha kwa kutupatia fedha,” alisema Balozi Mahiga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles